1Nawe mwana wa mtu, jipatie upanga mkali, uutumie kuwa wembe wa kinyozi wa kunyolea kichwa chako na udevu wako! Kisha jipatie mizani, uzigawanye hizo nywele!
2Fungu la tatu uliteketeze kwa moto mjini katikati, siku za kusongwa zitakapomalizika! Fungu la tatu jingine lichukue, ulitapanye na kupigapiga kwa upanga ukizunguka mjini po pote! Nalo fungu la tatu jingine utalitupatupa kwenye upepo, nami nitauchomoa upanga, uzifuata nyuma.
3Nawe hizo nywele zichukue chache tu, uzifungue pembeni katika vazi lako!
4Namo uchukue tena kidogo, uzitupe penye ule moto unaowaka mjini katikati, uziteketeze mle motoni! Ndimo, utakamotoka moto wa kuula mlango wote wa Isiraeli.
5Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Huu ndio Yerusalemu! Nimeuweka kwenye wamizimu katikati, ukazungukwa na nchi zao.
6Lakini kwa kuwa haukunicha, uliyakataa mashauri yangu kuliko hao wamizimu, ukayakataa nayo maongozi yangu kuliko hizo nchi ziuzungukazo, kwani mashauri yangu wakayabeua, hawakuyafuata maongozi yangu.
7Kwa sababu hii Bwana Mungu anasema hivi: Kwa kuwa mnafanya matata kuliko wamizimu wanaowazunguka, msipoyafuata maongozi yangu, wala msipoyafanya mashauri yangu, wala msipoyafanya maamuzi yangu, wamizimu wawazungukao wanayoyafanya,
8kwa hiyo Bwana Mungu anasema hivi: Utaniona, mimi nami nikikujia, nifanye katikati yako mashauri machoni pa wamizimu.
9Nitakufanyizia mambo, nisiyoyafanya bado, wala sitayafanya mara nyingine yaliyo hivyo kwa ajili ya machukizo yako yote.
10Nayo ni haya: katikati yako baba watakula wana, nao wana watakula baba zao! Haya ndiyo mashauri, nitakayokufanyizia, kisha masao yako nitayatupiatupia pande zote za upepo.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.