Waefeso 3 - Swahili Roehl Bible 1937

Ufunuo wa fumbo la Mungu.

1Hayo yamenipeleka mimi Paulo kifungoni kuwa mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi wamizimu.

13Kwa hiyo naomba, msichoke kwa ajili ya maumivu yangu, niliyopatwa nayo kwa ajili yenu, maana yanawapatia utukufu.

14Kwa sababu hii nampigia Baba na Bwana wetu Yesu Kristo magoti;

15kwani kila aliye baba, kama yuko mbinguni au yuko nchini, hujiita na jina hili la baba.

16Nawaombea, kwa wingi wa utukufu wake awape, mtu wenu wa ndani apate nguvu akikuzwa na Roho wake.Ef. 1:7; 6:10.

17Tena awape, Kristo akae mioyoni mwenu kwa hivyo, mnavyomtegemea, mpate kushusha mizizi katika upendo, mshikizwe nayo!Yoh. 14:23; Kol. 2:7.

18Kisha awape, mweze kupima pamoja na watakatifu wote, upendo ulivyo mpana na mrefu, tena unavyoingia chini, hata unavyokwenda juu;

19ndivyo, mtakavyoutambua upendo wake Kristo, ya kuwa unaupita utambuzi wote, mpate kuujaa katika mambo yote, kama Mungu alivyoujaa.

20Lakini yeye kwa hivyo, nguvu yake inavyokaza mwetu, anaweza kufanya kuyapita yote, tuyaombayo nayo tuyawazayo,

21yeye atukuzwe kwao wateule walio wake Kristo Yesu siku zote zitakazokuwapo kale na kale pasipo mwisho! Amin.*

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help