1Bwana akamwambia Mose: Jichongee mbao mbili za mawe, kama zile za kwanza zilivyokuwa! Nami nitaziandika hizo mbao maneno yale yaliyokuwa katika zile mbao za kwanza, ulizozivunja.(18-26: 2 Mose 23:14-19.)
17Usijifanyizie miungu kwa kuyeyusha yo yote.Uso wa Mose unaangaza.
29Ikawa, Mose aliposhuka mlimani kwa Sinai alizishika hizo mbao mbili za Ushahidi mkononi mwake na kushuka mlimani kwa Sinai; hapo yeye Mose alikuwa hajui, ya kama ngozi ya uso wake inaangaza kwa kusema na Bwana.
30Haroni na wana wa Isiraeli walipomwona Mose, mara wakaona, ya kama ngozi ya uso wake inaangaza; ndipo, walipoogopa kumkaribia.2 Kor. 3:7-18.
31Mose alipowaita, wakarudi kwake, Haroni nao watu wote walio wakuu penye mkutano wakarudi kwake, naye Mose akasema nao.
32Baadaye wana wote wa Isiraeli wakamkaribia, akawaagiza yote, Bwana aliyomwambia mlimani kwa Sinai.
33Mose alipokwisha kusema nao akaufunika uso wake kwa mharuma.
34Lakini Mose alipomtokea Bwana kusema naye akauondoa huo mharuma, mpaka atoke kwake. Naye alipotoka kwake, aseme na wana wa Isiraeli na kuwaambia aliyoagizwa,2 Mose 33:8-9.
35wana wa Isiraeli wakauona uso wake, ya kuwa uso wa Mose unaangaza; ndipo, Mose alipourudisha mharuma usoni pake, mpaka aingie tena kusema na Bwana.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.