Waebureo 11 - Swahili Roehl Bible 1937

Kumtegemea Mungu kulivyo.

1Kumtegemea Mungu ni kuyatumaini, tunayoyangojea, pasipo kuyaonea mashaka yasiyonekana bado.Jinsi Abeli na Henoki na Noa walivyomtegemea Mungu.

3Kwa kumtegemea Mungu twajua, ya kuwa ulimwengu ulitengenezwa kwa Neno lake Mungu, mtu asiseme: Tunavyoviona kwa macho, vilipata kuwapo kwa nguvu yao vile vinavyoonekana.Jinsi Aburahamu na Sara walivyomtegemea Mungu.

8Kwa kumtegemea Mungu Aburahamu alitii alipoitwa, ahame, aende mahali, atakapopewa kuwa urithi wake. Akahama, asijue, aendako.Jinsi wakale tangu Aburahamu walivyomtegemea Mungu.

17Kwa kumtegemea Mungu Aburahamu alipojaribiwa alimtoa Isaka, awe ng'ombe ya tambiko, yeye aliyekuwa mwana wake wa pekee.Nguvu ya kumtegemea Mungu huoneka katika mateso.

32Nisemeje tena? Kwani saa hazingenitosha, kama ningeyasimulia mambo ya Gideoni na ya Baraka na ya Samusoni na ya Yefuta na ya Dawidi na ya Samweli na ya wafumbuaji.Amu. 4:6; 6:11; 12:7; 15:20; 1 Sam. 3.

33Hao kwa kumtegemea Mungu walipigana na wafalme, wakawashinda, wakaamua kwa wongofu, wakaona, viagio vilivyotimia, wakavifunga vinywa vya simba,Amu. 14:6; 1 Sam. 17:34-35; Dan. 6:22.

34wakazima mioto yenye nguvu, wakapona ukali wa panga. Walipokuwa wanyonge walipewa nguvu tena, wakawa wakali vitani, wakakimbiza vikosi vizima vya wageni.Dan. 3:23-25.

35Kwa kufufuka kwao, ambao walifiwa nao, wanawake waliwapata tena wao hao, waliofiwa nao. Lakini wengine walipoteswa walitaka kuuawa, wakakataa kukombolewa, wapate ufufuko ulio mzuri uliko huo.1 Fal. 17:23; 2 Fal. 4:36.

36Wengine walijaribiwa na kufyozwa pamoja na kupigwa, wengine wakafungwa minyororo, wakatiwa vifungoni.Yer. 20; 37; 38.

37Waliuawa kwa kupigwa mawe, walipondwa, walipasuliwa, walikufa kwa kuchomwa majisu, walifukuzwa po pote, wajiendee wakivaa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi tu, wakiwa na njaa, wakiumia kwa maovu, waliyofanyiziwa.2 Mambo 24:21.

38Kweli haikuupasa ulimwengu huu kuwa nao, wakatangatanga maporini na milimani na mapangoni na mashimoni ndani ya nchi.

39Hao wote walipoteseka, ndipo, walipotimiza kumtegemea Mungu, lakini hawakuona, kiagio kilivyotimia.

40Kwani Mungu alikuwa ametupatia kale kitu kilicho kizuri sana, maana wale wasipate kutimilika pasipo sisi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help