Ufunuo 18 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Kuanguka kwa Babeli

1 Ufu 10:1; Eze 43:2 Baada ya hayo niliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, akiwa na mamlaka makuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.

2Isa 13:21; 21:9; 34:11; Yer 9:11; 50:39; 51:8; Ufu 14:8; Dan 4:30 Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ulio mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;

3Isa 23:17; Yer 25:15,27; 51:7; Nah 3:4 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.

4 Isa 48:20; 52:11; Yer 50:8; 51:6,9,45 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.

5Mwa 18:20-21; Yer 51:9 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.

6Zab 137:8; Yer 50:15,29; 2 The 1:6 Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni mara mbili.

7Isa 47:7-9; Yer 50:29 Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri hiyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia, wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe.

8Isa 47:9; Yer 50:34; Ufu 17:16 Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu.

9 Eze 26:16-17 Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake;Eze 27:30-35; Isa 23:17; Ufu 17:2

10Dan 4:30; Eze 26:17; Isa 21:9; Yer 51:8; Ufu 14:8 wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.

11Eze 27:31,36 Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;

12Eze 27:12-13,22 bidhaa ya dhahabu, fedha, vito vyenye thamani, lulu, kitani nzuri, nguo ya rangi ya zambarau, hariri na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, kila chombo cha pembe, kila chombo cha mti wa thamani nyingi, cha shaba, cha chuma na cha marimari;

13Eze 27:13 na mdalasini, iliki, uvumba, marhamu, ubani, mvinyo, mafuta ya mzeituni, unga mzuri na ngano, ng'ombe na kondoo, farasi na magari, na miili na roho za wanadamu.

14Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fahari vimekupotea; wala watu hawataviona tena kamwe.

15 Eze 27:31,36 Na wafanya biashara ya vitu hivyo, waliopata mali kwake, watasimama mbali, kwa hofu ya maumivu yake; wakilia na kuomboleza,

16Ufu 17:4 wakisema, Ole, ole, mji ule mkuu! Uliovikwa kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na nguo nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu, na vito vya thamani, na lulu;

17Isa 23:14; Eze 27:26-30 kwa kuwa katika saa moja utajiri mwingi namna hii umekuwa ukiwa. Na kila nahodha na kila aendaye mahali popote kwa matanga, na mabaharia, nao wote watendao kazi baharini, wakasimama mbali;

18Eze 27:32; Isa 34:10 wakalia sana, walipouona moshi wa kuungua kwake, wakisema, Ni mji upi ulio kama mji huu mkubwa!

19Eze 26:19; 27:30-34 Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu baharini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa.

20Kum 32:43; Yer 51:48; Isa 44:23 Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.

21 Yer 51:63-64; Eze 26:21; Dan 4:30 Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa.

22Eze 26:13; Isa 24:8 Wala sauti ya wapiga vinanda, na ya wapiga zomari, na ya wapiga filimbi, na ya wapiga baragumu, haitasikika ndani yako tena kabisa; wala fundi awaye yote wa kazi yoyote hataonekana ndani yako tena kabisa; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikiwa ndani yako tena kabisa;Yer 7:34; 25:10

23Yer 7:34; 16:9; 25:10; Isa 23:8; 47:9 wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa; wala sauti ya bwana harusi na bibi harusi haitasikika ndani yako tena kabisa; maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako.

24Yer 51:9,49; Mt 23:35; Ufu 6:10; 17:6; 19:2 Na ndani yake ilionekana damu ya manabii, na ya watakatifu, na ya wale wote waliouawa juu ya nchi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help