1 Mk 1:12,13; Lk 4:1-13 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.Ebr 2:18; 4:15
2Kut 34:28; 1 Fal 19:8 Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwishowe akaona njaa.
3Mwa 3:1-7 Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.
4Kum 8:3 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
5Mt 27:53 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,
6Zab 91:11-12 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini; kwa maana imeandikwa,
Atakuagizia malaika zake;
Na mikononi mwao watakuchukua;
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7 Kum 6:16 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka katika mlima mrefu mno, akamwonesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
9akamwambia, Haya yote nitakupa, ukiinama na kunisujudia.
10Kum 6:13 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.
11Yn 1:51; Ebr 1:6,14 Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.
Yesu anaanza huduma yake katika Galilaya12 Mk 1:14,15; Lk 4:14,15 Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya;Mt 14:3; Mk 6:17; Lk 3:19-20
13Yn 2:12 akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali;
14Isa 8:13; 9:1 ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,
15 Isa 8:13–9:1 Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,
Njia ya bahari, ng'ambo ya Yordani,
Galilaya ya mataifa,
16Watu wale waliokaa katika giza
Wameona mwanga mkuu,
Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti
Mwanga umewazukia.
17 Mt 3:2 Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
Yesu anawaita wanafunzi wa kwanza18 Mk 1:16-20; Lk 5:1-11 Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.Yn 1:40
19Mt 13:47; Eze 47:10 Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.
20Mt 19:27 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
21Alipoendelea, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwa katika mashua pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita.
22Mara wakaiacha mashua na baba yao, wakamfuata.
Yesu awahudumia makundi ya watu23 Mt 9:35; Mk 1:39; Lk 4:15,44; Mdo 10:38 Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila namna waliyokuwa nayo watu.
24Mk 6:55 Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
25Mk 3:7,8; Lk 6:17-19 Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Yudea, na ng'ambo ya Yordani.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.