1
4 Mwa 28:10-22 Naam, alishindana na malaika
Akashinda; alilia, na kumsihi;
Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;
5Naam, BWANA, Mungu wa majeshi;
BWANA ndilo kumbukumbu lake.
6Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.
7Ni mfanya biashara, aliye na mizani ya udanganyifu mkononi mwake; anapenda kudhulumu.
8Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wowote uliokuwa dhambi.
9Law 23:42-43 Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za sikukuu teule.
10Tena nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa utumishi wa manabii nimetumia mifano.
11Amo 4:4 Katika Gileadi kuna uovu? Nao wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng'ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.
12 Mwa 29:1-20 Na Yakobo alikimbia mpaka Padan-Aramu,
Na Israeli alitumika apate mke;
Ili apate mke alichunga kondoo.
13 Kut 12:50-51 Na kwa nabii BWANA alimtoa Israeli katika Misri,
Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.
14 Kum 28:37; Dan 11:18 Efraimu amenitia hasira kali sana; kwa sababu hiyo damu yake itaachwa juu yake, na Bwana wake atamrudishia lawama yake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.