1Samweli 11 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Sauli awashinda Waamoni

1 Mwamoni, akakwea na kupiga kambi juu ya Yabesh-gileadi; na watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, Fanya mapatano nasi, na sisi tutakutumikia.

2Mwa 34:14; 1 Sam 17:26 Huyo Nahashi, Mwamoni, akawaambia, Kwa sharti hili mimi nitapatana nanyi, kila mtu ang'olewe jicho la kulia; na kwa jambo hilo nitawashutumu Waisraeli wote pia.

3Basi wazee wa Yabeshi wakamjibu, Tuachie siku saba, ili tutume wajumbe waende kote mipakani mwa Israeli; kisha, ikiwa hakuna atakayetuokoa, tutajisalimisha kwako.

41 Sam 10:26; 14:2; 2 Sam 21:6; Amu 2:4; 21:2; Rum 12:15 Hivyo wajumbe wakafika Gibea ya Sauli, wakasema maneno hayo masikioni mwa watu; na watu wote wakainua sauti zao wakalia.

5Na tazama, Sauli akaja akifuata ng'ombe kutoka kondeni; naye Sauli akauliza, Watu hawa wana nini, hata wakalia? Wakamwambia maneno ya watu wale wa Yabeshi.

6Amu 3:10; 6:34; 11:29; 13:25; 14:6; 1 Sam 10:10; 16:13 Na Roho ya Mungu ikamjia Sauli kwa nguvu, hapo alipoyasikia maneno yale, na hasira yake ikawaka sana.

7Amu 19:29; 21:5; Mwa 35:5; 2 Nya 14:14; 17:10; Mit 14:26; Amu 20:1 Akachukua fahali wawili waliofungwa nira, akawakatakata vipande, kisha akawatuma wajumbe kuvipeleka vile vipande kote katika Israeli, wakisema, Yeyote ambaye hatamfuata Sauli na Samweli, ng'ombe wake watafanyiwa vivi hivi. Basi utisho wa BWANA ukawaangukia wale watu, wakatoka kwa pamoja.

8Amu 1:5; 2 Sam 24:9 Naye akawahesabu huko Bezeki; Waisraeli walikuwa elfu mia tatu, na Wayuda elfu thelathini.

9Nao wakawaambia hao wajumbe waliokuja, Waambieni watu wa Yabesh-gileadi, Kesho, wakati wa jua kali, mtapata wokovu. Basi wale wajumbe wakaenda, wakawaarifu watu wa Yabeshi; nao wakafurahi.

10Kwa hiyo watu wa Yabeshi walisema, Kesho tutawatokea, nanyi mtatufanyia yote myaonayo kuwa ni mema.

111 Sam 31:11; Amu 7:16; Yak 2:13 Ikawa, kesho yake, Sauli akawapanga watu katika vikosi vitatu; nao wakaingia katikati ya kambi kwenye zamu ya asubuhi, wakawapiga Waamoni hadi wakati wa jua kali; kisha ikawa wale waliosalia wakatawanyika, hata wasiachwe wawili wao pamoja.

121 Sam 10:27; Zab 21:8; Lk 19:27 Ndipo watu walipomwambia Samweli, Ni nani yule aliyesema, Je! Huyo Sauli atatutawala? Walete watu hao, ili tuwaue.

132 Sam 19:22; Kut 14:13,30; 1 Sam 14:45; 19:5; 1 Nya 11:14; Zab 44:4-8; Ebr 2:3 Lakini Sauli akasema, Hakuna mtu atakayeuawa leo, maana leo BWANA amefanya wokovu katika Israeli.

14 1 Sam 10:8 Kisha Samweli akawaambia watu, Haya! Na twendeni mpaka Gilgali, ili tuuanzishe ufalme upya huko.

15Nao watu wote wakaenda Gilgali; wakamtawaza Sauli mbele za BWANA huko Gilgali; wakachinja sadaka za amani mbele za BWANA; na huko Sauli na watu wote wa Israeli wakafurahi sana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help