Ezekieli 25 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Tangazo juu ya Amoni

1 Yer 49:1-6; Eze 21:28-32; Amo 1:13-15; Sef 2:8-11 Neno la BWANA likanijia, kusema,

2Yer 49:1; Amo 1:13; Sef 2:9 Mwanadamu, uwaelekezee wana wa Amoni uso wako, ukatabiri juu yao.

3Mit 17:5 Uwaambie hao wana wa Amoni, Lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umesema, Aha! Juu ya patakatifu pangu, palipotiwa unajisi; na juu ya nchi ya Israeli, ilipoharibiwa; na juu ya nyumba ya Israeli, walipokwenda kifungoni;

4Mwa 45:18 basi, kwa sababu hiyo, nitakutia katika mikono ya wana wa mashariki uwe milki yao, nao watajenga kambi yao ndani yako, kufanya maskani zao ndani yako; watakula matunda yako, na kunywa maziwa yako.

52 Sam 12:26; Isa 13:21; Eze 21:20; Sef 2:14 Nami nitafanya Raba kuwa banda la ngamia, na wana wa Amoni kuwa mahali pa kulaza makundi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.

6Maana Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umepiga makofi, na kupiga mshindo kwa miguu yako, na kufurahi juu ya nchi ya Israeli, jeuri yote ya roho yako;

7basi, tazama, nimenyosha mkono wangu juu yako, nami nitakutoa uwe mateka ya mataifa; nami nitakukatilia mbali na makabila ya watu, nami nitakuangamiza, usiwe katika nchi hizo; nitakukomesha; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.

Utabiri juu ya Moabu

8 Kum 2:4,5; Isa 15:1–16:14; 25:10-12; Yer 48:1-47; Amo 2:1-3; Sef 2:8-11 Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu Moabu na Seiri husema, Tazama, nyumba ya Israeli ni sawasawa na mataifa yote;

9basi, tazama, nitawafunulia wana wa mashariki ubavu wa Moabu toka miji yake, toka miji yake iliyo mipakani mwake, utukufu wa nchi hiyo, Beth-yeshimothi, na Baal-meoni, na Kiriathaimu,

10pamoja na wana wa Amoni, nami nitawatoa kuwa milki, ili wana wa Amoni wasikumbukwe kati ya mataifa,

11nami nitatoa hukumu juu ya Moabu; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.

Utabiri juu ya Edomu

12 2 Nya 28:17; Zab 137:7; Omb 4:22; Isa 34:5-17; 63:1-6; Yer 49:7-22; Eze 35:1-15; Amo 1:11-12; Oba 1:1-14; Mal 1:2-5 Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Edomu wametenda kinyume cha nyumba ya Yuda, kwa kujilipiza kisasi, nao wamekosa sana, na kujilipiza kisasi juu yao;

13kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Nitanyosha mkono wangu juu ya Edomu, nitakatilia mbali nayo wanadamu na wanyama; nami nitaifanya kuwa ukiwa toka Temani; na mpaka Dedani wataanguka kwa upanga.

14Isa 11:14 Nami nitaweka kisasi changu juu ya Edomu, kwa mkono wa watu wangu Israeli; nao watatenda mambo katika Edomu, kwa kadiri ya hasira yangu, na ghadhabu yangu, nao watakijua kisasi changu, asema Bwana MUNGU.

Utabiri juu ya Filistia

15 Isa 14:29-31; Yer 47:1-7; 25:20; Yoe 3:4-8; Amo 1:6-8; Sef 2:4-7; Zek 9:5-7 Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Wafilisti wametenda mambo kwa kujilipiza kisasi, nao wamejilipiza kisasi kwa moyo wa ujeuri, ili kupaangamiza kwa uadui wa daima;

161 Sam 30:14 kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitanyosha mkono wangu juu ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi, na kuwaharibu wabakio pande za pwani.

17Zab 9:16; Isa 26:11; Eze 6:7 Nami nitajilipiza kisasi kikuu, nikiwakemea kwa ukali; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapojilipiza kisasi juu yao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help