Ezekieli 14 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Hukumu za Mungu zathibitishwa

1 Eze 8:1; 20:1 Ndipo baadhi ya wazee wa Israeli wakanijia, wakaketi mbele yangu.

2Ndipo neno la BWANA likanijia, kusema,

3Eze 3:20; 7:19; 1 Pet 2:8; Ufu 2:14; Mit 15:8 Mwanadamu, watu hawa wametwaa vinyago vyao na kuvitia mioyoni mwao, nao wameweka kwazo la uovu wao mbele ya nyuso zao. Je! Nitakubali kuombwa ushauri na wao?

4Basi sema nao, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Kila mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea nabii; mimi, BWANA, nitamjibu neno lake kulingana na wingi wa sanamu zake;

5Ebr 3:12-19 ili niwakamate nyumba ya Israeli kwa mioyo yao wenyewe, kwa sababu wamefarakana nami kwa vinyago vyao.

6Kwa sababu hiyo uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Rudini ninyi, mkageuke na kuviacha vinyago vyenu; mkageuze nyuso zenu zisielekee machukizo yenu yote.

7Yer 2:13; Mt 6:24; Yud 1:19 Kwa maana kila mtu wa nyumba ya Israeli, au wa wageni wakaao katika Israeli, ajitengaye nami, na kuvitwaa vinyago vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, kisha kumwendea nabii, na kuniuliza neno kwa ajili ya nafsi yake; mimi, BWANA, nitamjibu, mimi mwenyewe;

8Law 17:10; Yer 44:11; Eze 15:7; 5:15; Hes 26:10; Kum 28:37 nami nitaukaza uso wangu juu ya mtu yule, na kumfanya kuwa ajabu, awe ishara na mithali, nami nitamkatilia mbali, asiwe kati ya watu wangu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.

9Ayu 12:16; Yer 4:10; 2 The 2:11 Na nabii akidanganyika, na kusema neno, mimi, BWANA, nimemdanganya nabii yule, nami nitaunyosha mkono wangu juu yake, na kumwangamiza, asiwe kati ya watu wangu Israeli.

10Nao watauchukua uovu wao; uovu wa nabii utakuwa sawasawa na uovu wake yule amwendeaye aulize neno;

11Zab 119:67,71; Ebr 12:11; Yer 31:18,19; 2 Pet 2:15; Yer 24:7; 30:22; 32:38; Eze 11:20; 36:28 ili nyumba ya Israeli wasipotee mbali nami, wala wasijitie unajisi tena kwa makosa yao yote; bali wawe watu wangu, nami niwe Mungu wao, asema Bwana MUNGU.

12Neno la BWANA likanijia, kusema,

13Law 26:26; Isa 3:1; Eze 4:16 Mwanadamu, nchi itakapofanya dhambi na kuniasi, kwa kukosa, nikaunyosha mkono wangu juu yake, na kulivunja tegemeo la chakula chake, na kuiletea njaa, na kukatilia mbali mwanadamu na mnyama;

14Yer 15:1; 7:16; Mit 11:4; 2 Pet 2:9 wajapokuwa watu hawa watatu, Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kuwamo ndani yake, wangejiokoa nafsi zao wenyewe tu kwa haki yao, asema Bwana MUNGU.

15Hes 21:6; Law 26:22 Nikipitisha wanyama wabaya ndani ya nchi ile, wakaiharibu hata ikawa ukiwa, mtu awaye yote asiweze kupita ndani yake, kwa sababu ya wanyama hao;

16wajapokuwamo watu hawa watatu ndani yake, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hawataokoa wana wala binti; wao wenyewe tu wataokoka, bali nchi ile itakuwa ukiwa.

17Law 26:25; Yer 33:12; Eze 5:12; 25:13; Hos 4:3 Au nikileta upanga juu ya nchi ile, na kusema, Upanga, pita kati ya nchi hii, hata nikawakatilia mbali na nchi hiyo wanadamu na wanyama;

18wajapokuwamo watu hawa watatu ndani yake, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hawataokoa wana wala mabinti; bali wao wenyewe tu wataokoka.

192 Sam 24:15; Eze 7:8; Ufu 16:3-6 Au nikituma tauni katika nchi ile, na kumwaga ghadhabu yangu juu yake, kwa damu; ili kuwakatilia mbali nayo wanadamu na wanyama;

20wajapokuwamo ndani yake Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hawangeokoa watoto wa kiume au wa kike; watajiokoa nafsi zao tu kwa haki yao.

21Yer 15:2,3; Eze 5:17; Amo 4:10; Ufu 6:8 Maana Bwana MUNGU asema hivi; Je! U zaidi sana nitakapoleta hukumu zangu nne zilizo kali juu ya Yerusalemu, yaani, upanga, na njaa, na wanyama wabaya, na tauni, niwakatilie mbali nayo wanadamu na wanyama?

22Eze 6:8; 20:43 Lakini, tazama, watasalia mabaki watakaochukuliwa nje, wana na mabinti; tazama, watawatokea ninyi, nanyi mtaiona njia yao na matendo yao; nanyi mtafarijika katika habari ya mabaya niliyoleta juu ya Yerusalemu, naam, katika habari ya mambo yote niliyoleta juu yake.

23Yer 22:8,9 Nao watawafariji ninyi, mtakapoona njia yao na matendo yao; nanyi mtajua ya kuwa sikufanya bila sababu mambo yote niliyoutenda, asema Bwana MUNGU.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help