1Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
2Katika wana wa Lawi uitenge hesabu ya wana wa Kohathi, kwa jamaa zao, na nyumba za baba zao,
3 kwa hilo pazia;
6 ya kulifunikia, na kutandika juu yake nguo ya rangi ya samawati tupu, kisha watatia hiyo miti yake.
7 za kuifunikia, na kuiweka ile miti yake.
9 na kukiweka juu ya miti ya kukichukulia
11 na kuitia ile miti yake;
12kisha watavitwaa vile vyombo vyote vya utumishi wavitumiavyo katika mahali patakatifu, na kuvitia katika nguo ya rangi ya samawati, na kuvifunika kwa ngozi za pomboo, na kuvitia juu ya miti ya kuvichukulia.
13Nao watayaondoa hayo majivu madhabahuni; na kutandika nguo ya rangi ya zambarau juu yake;
14nao wataweka vyombo vyake vyote juu yake ambavyo wavitumia katika madhabahu, vyetezo, na nyuma, na miiko, na mabakuli, vyombo vyote vya hiyo madhabahu; nao watatandika juu yake ngozi za pomboo, na kutia miti yake mahali pake.
15Hes 7:9; 10:21; Kum 31:9; 2 Sam 6:13; 1 Nya 15:2,15; 2 Sam 6:6,7; 1 Nya 13:9,10; Hes 3:31 Na Haruni na wanawe watakapokwisha kupafunika mahali patakatifu, na vyombo vyote vya mahali patakatifu, hapo watakapong'oa kambi; baadaye, wana wa Kohathi watakuja kuvichukua; lakini wasiviguse vile vitu vitakatifu, wasife. Vyombo vile ni mzigo wa wana wa Kohathi katika hema ya kukutania.
16Kut 25:6; 30:34; Zab 141:2; Mal 1:11; Ufu 5:8; 8:3; Kut 29:40; Hes 28:3; Kut 30:23 Na ulinzi wake Eleazari mwana wa Haruni kuhani utakuwa ni kuyaangalia mafuta ya nuru, na uvumba mzuri, na sadaka ya unga ya daima, na mafuta ya kupaka, tena ulinzi wa hiyo maskani yote, na wa vitu vyote vilivyo ndani yake, mahali patakatifu, na vyombo vyake.
17Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
18Msilitenge kabisa kabila la jamaa za Wakohathi katika hao Walawi;
19Hes 4:4 lakini wafanyieni neno hili, ili kwamba wawe hai, wasife, hapo watakapovikaribia vile vitu vilivyo vitakatifu sana; Haruni na wanawe wataingia ndani, na kuwawekea kila mtu utumishi wake, na kila mtu mzigo wake;
20Kut 19:21; 1 Sam 6:19 lakini wasiingie wao kupaona mahali pale patakatifu, hata kwa dakika moja, ili wasife.
Wagershoni na Wamerari21Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
22Fanya hesabu za wana wa Gershoni nao, kwa nyumba za baba zao, na jamaa zao;
231 Nya 23:3,24,27 tangu waliopata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini utawahesabu; wote watakaoingia kutumika, ili kufanya kazi katika hema ya kukutania.
24Huu ni utumishi wa jamaa za Wagershoni, katika kutumika na katika kuchukua mizigo;
25Kut 26:1-14; 38:9; 40:19; Hes 3:25,26 wao watayachukua mapazia ya Hema Takatifu, na hema ya kukutania, hizo nguo za kufunikia, na zile ngozi za pomboo za kufunikia zilizo juu yake, na pazia la mlango wa hema ya kukutania;
26na pazia za nguo za ua, na sitara ya ile nafasi ya kuingilia ya lango la ua, ulio karibu na maskani na madhabahu, kuzunguka pande zote, na kamba zake, na vyombo vyote vya utumishi wao, na yote yatakayotendeka kwavyo, watatumika katika hayo.
27Utumishi wote wa wana wa Wagershoni, katika mzigo wao wote, na utumishi wao wote, utakuwa kwa amri ya Haruni na wanawe; nanyi mtawaagizia mzigo wao wote kuulinda.
28Huu ni utumishi wa jamaa za wana wa Wagershoni katika hema ya kukutania; na ulinzi utakuwa chini ya mkono wa Ithamari mwana wa Haruni kuhani.
29Katika habari ya wana wa Merari, utawahesabu kwa jamaa zao, na nyumba za baba zao;
30Mwa 41:46; Hes 4:23; 8:24; 1 Nya 28:12,13 tangu aliyepata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini, utawahesabu, kila atakayeingia katika huo utumishi, ili kufanya kazi ya hema ya kukutania.
31Hes 3:36,37; Kut 26:15; 27:9-19 Na mausia ya mzigo wao ni haya, kwa utumishi wao wote katika hema ya kukutania; mbao za Hema Takatifu, na mataruma yake, na nguzo zake, na vitako vyake;
32Kut 25:9; 1 Nya 9:29; Ezr 8:24-30 na viguzo vya ua vya kuuzunguka pande zote, na vitako vyake, na vigingi vyake, na kamba zake, na vyombo vyake vyote, pamoja na utumishi wake wote; nanyi mtawaagizia kila mtu kwa jina lake vile vyombo vya mzigo wao watakaoulinda.
33Huu ni utumishi wa jamaa za wana wa Merari, kwa utumishi wao wote, katika hema ya kukutania, chini ya mkono wa Ithamari mwana wa Haruni kuhani.
Hesabu ya Walawi34 Hes 3:19,27; 4:2 Basi Musa na Haruni na hao wakuu wa mkutano wakawahesabu wana wa Kohathi kwa jamaa zao, na nyumba za baba zao,
35Hes 8:24-26; 1 Nya 23:24; 28:13; Lk 3:23; 1 Tim 3:6 tangu waliopata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini, kila mtu aliyeingia katika utumishi kwa kazi katika hema ya kukutania,
36na waliohesabiwa kwao kwa jamaa zao, walikuwa elfu mbili na mia saba hamsini.
37Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za Wakohathi, wote waliotumika katika hema ya kukutania, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA kwa mkono wa Musa.
38Na hao waliohesabiwa katika wana wa Gershoni, kwa jamaa zao na nyumba za baba zao,
39kuanzia wenye umri wa miaka thelathini na zaidi, hadi umri wa miaka hamsini, kila mtu aliyeingia katika utumishi, kwa kazi katika hema ya kukutania,
40hata wale waliohesabiwa kwao, kwa jamaa zao na nyumba za baba zao, walikuwa elfu mbili na mia sita na thelathini.
41Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za wana wa Gershoni, wote waliotumika katika hema ya kukutania, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA.
42Na hao waliohesabiwa katika jamaa za wana wa Merari, kwa jamaa zao, na nyumba za baba zao,
43Hes 4:35-40; Kum 33:25; 1 Kor 12:8-12; 2 Kor 12:9 kuanzia wenye umri wa miaka thelathini na zaidi, hadi umri wa miaka hamsini, kila mtu aliyeingia katika utumishi kwa kazi katika hema ya kukutania,
44wale waliohesabiwa kwao, kwa jamaa zao, walikuwa elfu tatu na mia mbili.
45Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za wana wa Merari, ambao Musa na; Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA, kwa mkono wa Musa.
46Wote waliohesabiwa katika Walawi, ambao Musa na Haruni na hao wakuu wa Israeli waliwahesabu, kwa jamaa zao, na nyumba za baba zao,
47Rum 12:6-8 tangu waliopata umri wa miaka thelathini na zaidi, hata umri wa miaka hamsini, kila aliyeingia kufanya kazi ya utumishi, na kazi ya kuchukua mizigo katika hema ya kukutania,
48hao waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu nane na mia tano themanini.
491 Kor 12:4-28 Kwa amri ya BWANA, walihesabiwa kwa mkono wa Musa, kila mtu kwa utumishi wake, na kama mzigo wake ulivyokuwa; ndivyo walivyohesabiwa na yeye, kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.