1 1 Tim 4:1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
2Rum 1:29 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
3wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,
4Flp 3:19 wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;
5Mt 7:15,21; Rum 2:20; Tit 1:16 walio na utaua kwa nje, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
6Mt 23:14; Tit 1:11 Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za kila namna;
72 Tim 2:25 wakijifunza siku zote, ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa kweli.
8Kut 7:11,22; 1 Tim 6:5; 1:12 Na kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, vivyo hivyo na hawa wanapingana na ile kweli; ni watu walioharibika akili zao, wamekataliwa kwa mambo ya imani.
9Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama vile na upumbavu wa hao ulivyokuwa dhahiri.
Mausia ya Paulo kwa Timotheo10Bali wewe umeyafuata mafundisho yangu, na mwenendo wangu, na makusudi yangu, na imani, na uvumilivu,
11Mdo 13:14-52; 14:1-20; Zab 34:19 na upendo, na subira; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.
12Mt 16:24; Mdo 14:22 Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.
131 Tim 4:1 Lakini watu waovu na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.
142 Tim 2:2 Bali wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao;
15Yn 5:39; Zab 119:99 na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
162 Pet 1:19-21; Rum 15:4 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
171 Tim 6:11 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.