Zaburi 45 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Wimbo wa harusi ya kifalmeKwa mwimbishaji: kwa kufuata mtindo wa Yungiyungi. Wimbo wa Wakorahi; Wimbo wa Mapenzi.

1Moyo wangu umefurika kwa jambo jema,

Mimi nasema niliyomfanyia mfalme;

Ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.

2Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu;

Neema imemiminiwa midomoni mwako,

Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.

3Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari,

Utukufu ni wako na fahari ni yako.

4Katika fahari yako usitawi uendelee

Kwa ajili ya kweli, upole na haki

Na mkono wako wa kulia

Utakutendea mambo ya ajabu.

5Mishale yako ni mikali, katika mioyo ya adui za mfalme;

Watu huanguka chini yako.

6 wanakushawishi kwa zawadi,

Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako.

13 Ufu 19:7,8 Binti mfalme yumo ndani ana fahari tupu,

Mavazi yake ni ya nyuzi za dhahabu.

14Anapelekwa kwa mfalme

Na mavazi yaliyofumwa kwa uzuri.

Wanawali wenzake wanaomfuata,

Pia watapelekwa kwako.

15Watapelekwa kwa furaha na shangwe,

Na kuingia katika nyumba ya mfalme.

16 1 Pet 2:9; Ufu 1:6 Badala ya baba zako watakuwapo watoto wako,

Utawafanya kuwa wakuu katika nchi zote.

17 Isa 11:10; Mal 1:11 Jina lako nitalifanya kuwa kumbukumbu

Katika vizazi vyote.

Kwa hiyo mataifa watakushukuru

Milele na milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help