Yeremia 16 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Ukapera wa Yeremia na ujumbe

1Tena neno la BWANA likanijia, kusema,

2Mwa 19:14 Wewe hutaoa mke, wala hutakuwa na wana wala binti mahali hapa.

3Maana BWANA asema hivi, kuhusu habari za wana, na kuhusu habari za binti, wazaliwao mahali hapa, na kuhusu habari za mama zao waliowazaa, na kuhusu habari za baba zao waliowazaa, katika nchi hii;

4watakufa kwa maradhi mabaya; hawataliliwa, wala hawatazikwa; watakuwa kama samadi juu ya uso wa nchi; nao wataangamizwa kwa upanga, na kwa njaa; na mizoga yao itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi.

5Zab 78:64; Eze 24:17 Maana BWANA asema hivi, Usiingie ndani ya nyumba yenye matanga, wala usiende kuwaombolezea, wala kuwalilia; maana nimewaondolea watu hawa amani yangu, asema BWANA, hata fadhili zangu na rehema zangu.

6Kum 14:1; Isa 22:12 Wakubwa kwa wadogo wote pia watakufa katika nchi hii; hawatazikwa, wala watu hawatawalilia, wala kujikatakata kwa ajili yao, wala kujinyoa kwa ajili yao;

7Mit 3:6 wala watu hawatamega mkate kwa ajili yao, wakati wa kuomboleza, ili kuwafariji kwa ajili yao waliokufa; wala watu hawatawapa kikombe cha faraja, wanywe kwa ajili ya baba yao au mama yao.

8Wala usiingie ndani katika nyumba yenye karamu, kuketi pamoja nao, na kula na kunywa.

9Isa 24:7; Hos 2:11; Yer 7:34; 25:10; Ufu 18:23 Maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Mimi, mbele ya macho yenu, na katika siku zenu, nitaikomesha sauti ya furaha, na sauti ya kicheko, mahali hapa; sauti ya bwana harusi, na sauti ya bibi harusi.

10Kum 29:24; Yer 5:19; 13:22 Tena itakuwa, utakapowaonesha watu hawa maneno haya yote, nao wakakuambia, Mbona BWANA amenena juu yetu mabaya haya makuu? Uovu wetu ni uovu gani? Na dhambi yetu, tuliyomtenda BWANA, Mungu wetu, ni nini?

11Amu 2:12,13; 1 Fal 9:9; 2 Nya 7:22; Neh 9:26-29; Zab 106:35-41; Yer 5:7,9; Dan 9:10-12 Ndipo utakapowaambia, Ni kwa sababu baba zenu wameniacha mimi, asema BWANA, na kuwafuata miungu mingine, na kuwatumikia, na kuwaabudu, wakaniacha mimi, wasiishike torati yangu;

12Yer 7:26; 2 Tim 3:13 na ninyi mmetenda mabaya kupita baba zenu; maana angalieni, mnaenda kila mmoja wenu kwa ushupavu wa moyo wake mbaya, msinisikilize mimi;

13Law 18:27,28; Kum 4:26; 2 Nya 7:20; Yer 15:4 basi, kwa sababu hiyo, nitawatoeni katika nchi hii, na kuwaingiza katika nchi ambayo hamkuijua, wala ninyi wala baba zenu; na huko mtawatumikia miungu mingine mchana na usiku; kwa maana mimi sitawapa fadhili zangu hata kidogo.

Mungu atairejesha Israeli

14Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema BWANA, ambapo hawatasema tena, Aishivyo BWANA, aliyewaleta wana wa Israeli toka nchi ya Misri;

15lakini, Aishivyo BWANA, aliyewaleta wana wa Israeli toka nchi ya kaskazini, na toka nchi zote alikowafukuza; nami nitawarudisha katika nchi yao wenyewe niliyowapa baba zao.

16Amo 4:2; Hab 1:15 Tazama, asema BWANA, Nitatuma watu kuwaita wavuvi wengi, nao watawavua; na baada ya hayo nitatuma watu kuwaita wawindaji wengi, nao watawawinda, watoke katika kila mlima, na kila kilima, na pango za majabali.

17Ayu 34:21; Mit 5:21; Yer 32:19 Maana macho yangu yaziangalia njia zao zote, hawakufichwa uso wangu usiwaone, wala haukusitirika uovu wao macho yangu yasiuone.

18Mik 4:10; Eze 43:7 Nami kwanza nitawalipa uovu wao na dhambi zao maradufu, kwa kuwa wameitia unajisi nchi yangu, kwa mizoga ya vitu vyao vichukizavyo, na kuujaza urithi wangu kwa machukizo yao.

19Zab 18:2; 22:27; Isa 2:2; 44:10 Ee BWANA, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.

20Isa 37:19; Gal 4:8 Je! Mwanadamu ajifanyie miungu, wasio miungu?

21Basi, tazama, nitawajulisha, mara moja hii nitawajulisha, mkono wangu, na nguvu zangu; nao watajua ya kuwa, jina langu ni YEHOVA.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help