1Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yanayomhusu Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi;
2Ebr 4:15 awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe ana udhaifu;
3Law 9:7; 16:6 na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi.
4Kut 28:1 Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni.
5Zab 2:7; Mdo 13:33 Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia,
Ndiwe mwanangu,
Mimi leo nimekuzaa.
6 Zab 110:4; Ebr 7:1 Kama asemavyo mahali pengine,
Ndiwe kuhani milele
Kwa mfano wa Melkizedeki.
7 Mt 26:36-46; Mk 14:32-42; Lk 22:39-46 Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;
8Flp 2:8 na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata;
9Isa 45:17; Yn 17:1,5 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;
10kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.
Maonyo juu ya uasi11Yeye ambaye tuna maneno mengi ya kunena kuhusu habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia.
121 Kor 3:2; 1 Pet 2:2 Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu.
13Efe 4:14 Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga.
14Flp 1:10; Rum 16:19; Mwa 2:17 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoeshwa kupambanua mema na mabaya.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.