Zaburi 62 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Wimbo wa kusifia imani kwa Mungu pekeeKwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.

1Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa utulivu,

Wokovu wangu hutoka kwake.

2Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,

Ngome yangu, sitatikisika.

3 Isa 30:13 Hadi lini mtamshambulia mtu,

Mpate kumwua ninyi nyote pamoja?

Kama ukuta unaoinama,

Kama ua ulio tayari kuanguka,

4 Zab 28:3 Mpango wao ni kumwangusha tu mtu mwenye cheo;

Huufurahia uongo.

Kwa kinywa chao hubariki;

Kwa moyo wao hulaani.

5 Mik 7:7,10 Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa utulivu.

Maana tumaini langu hutoka kwake.

6Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,

Ngome yangu, sitatikisika.

7 Yer 3:23 Kwa Mungu wokovu wangu,

Na utukufu wangu;

Mwamba wa nguvu zangu,

Na kimbilio langu ni kwa Mungu.

8 1 Sam 1:15; Zab 42:4 Enyi watu, mtumainini siku zote,

Ifunueni mioyo yenu mbele zake;

Mungu ndiye kimbilio letu.

9Hakika binadamu ni ubatili,

Na wenye cheo ni uongo,

Katika mizani huinuka;

Wote pamoja ni hafifu kuliko ubatili.

10 Isa 26:4; Mk 10:23; Lk 12:15 Msiitumainie dhuluma,

Wala msijivune kwa unyang'anyi;

Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.

11Mara moja amenena Mungu;

Mara mbili nimeyasikia haya,

Ya kuwa nguvu zina Mungu,

12 Ayu 34:11; Yer 17:10; Mt 16:27; 1 Pet 1:17; Rum 2:6; Ufu 2:23 Na fadhili ziko kwako, Ee Bwana;

Maana ndiwe umlipaye kila mtu

Kulingana na haki yake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help