1 atawekwa hai mbele za BWANA ili kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka jangwani kwa ajili ya Azazeli.
11Na Haruni atamsongeza ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake; naye atamchinja yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake.
12
22Zab 103:1-13; Mt 8:17; Yn 1:29; Ebr 9:28; 1 Pet 2:24 Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyokaliwa na watu; kisha atamwacha aende jangwani.
23Eze 44:19; 42:14; Flp 2:6-11 Na Haruni ataingia katika hema ya kukutania, naye atavua mavazi yake ya kitani, aliyoyavaa alipoingia katika patakatifu, atayaacha humo;
24naye ataosha mwili wake kwa maji mahali patakatifu, na kuvaa nguo zake, na kutoka, na kusongeza sadaka ya kuteketezwa yake mwenyewe, na sadaka ya kuteketezwa ya watu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake, na kwa ajili ya watu.
25Kut 29:13; Law 4:10 Na mafuta ya sadaka ya dhambi atayateketeza juu ya madhabahu.
26Law 15:5; Ebr 9:10 Na mtu yule amwachaye mbuzi wa Azazeli aende zake, ataosha nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia katika kambi.
27Ebr 13:11; Law 8:17; 4:12; 6:30 Na yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, na yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, ambao damu yao ililetwa ndani ifanye ukumbusho katika patakatifu, watachukuliwa nje ya kambi; nao watateketeza ngozi zao, na nyama yao, na mavi yao.
28Na yeye awachomaye moto atafua nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia kambini.
29 Law 23:26-32; Hes 29:7-11; Kut 30:10; Isa 58:3,5; Dan 10:3,12 Amri hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba, siku ya kumi ya mwezi, mtajinyima, msifanye kazi ya namna yoyote, mzaliwa na mgeni akaaye kati yenu.
30Eze 36:25; Yer 33:8; Tit 2:14; Efe 5:26; Ebr 9:13,14; 1 Yoh 1:7,9 Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za BWANA.
31Kut 31:15; 35:2; Law 23:32; 25:4 Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajinyima; ni amri ya milele.
32Kut 29:29; Hes 20:26 Na kuhani atakayetiwa mafuta na kuwekwa wakfu badala ya baba yake, ataufanya huo upatanisho, naye atayavaa mavazi ya kitani, yaani, yale mavazi matakatifu.
33Naye atafanya upatanisho kwa ajili ya patakatifu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya hema ya kukutania, na kwa ajili ya madhabahu; naye atafanya upatanisho kwa ajili ya makuhani, na kwa ajili ya watu wote wa kusanyiko.
34Law 23:31; Hes 29:7; Kut 30:10; Ebr 9:7,25 Na amri hii itakuwa amri ya milele kwenu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya wana wa Israeli kwa sababu ya dhambi zao zote, mara moja kila mwaka. Naye akafanya vile vile kama BWANA alivyomwamuru Musa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.