Yeremia 45 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Neno la faraja kwa Baruku

1 2 Fal 24:1; 2 Nya 36:5-7; Dan 1:1-2; Isa 50:4; Yer 36:1-4,32 Neno hili ndilo ambalo Yeremia, nabii, alimwambia Baruku, mwana wa Neria, alipoyaandika maneno haya katika kitabu kwa kinywa cha Yeremia, mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, kusema,

2BWANA, Mungu wa Israeli, akuambia wewe Ee Baruku;

3Ulisema, Ole wangu! Kwa maana BWANA ameongeza huzuni pamoja na maumivu yangu. Nimechoka kwa ajili ya kuugua kwangu, wala sioni raha.

4Isa 5:5 Basi, mwambie hivi, BWANA asema hivi, Tazama, niliyoyajenga nitayabomoa, na niliyoyapanda nitayang'oa; na haya yatakuwa katika nchi yote.

5Zab 4:6; Mt 6:34; Mwa 6:12; Isa 66:16; Yer 21:9; 38:2 Je! Unajitafutia mambo makuu? Usiyatafute; kwa maana tazama, nitaleta mabaya juu ya wote wenye mwili, asema BWANA; lakini roho yako nitakupa iwe nyara, katika mahali pote utakapokwenda.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help