Tobiti 9 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

NDOA YA TOBIAFedha zarudishwa

1Kwa hiyo Tobia akamwita Rafaeli, akamwambia,

2Ndugu yangu Azaria, utwae mtumishi mmoja na ngamia wawili, uende Rage, mji wa Umedi,

3kwa Gabaeli, ili uniletee ile fedha; tena uje naye kwenye karamu ya harusi. Yaani, Ragueli ameapa nisiondoke mimi.

4Ati! Baba yangu anazihesabu siku, nami nikikawia sana atahuzunika mno.

5Hivyo Rafaeli akaondoka, akaenda akatua kwa Gabaeli, akampa ile hati. Naye akaileta ile mifuko ya fedha yenye mihuri yake, akampa.

6Asubuhi mapema wakaondoka wote wawili wakafika kwenye karamu ya harusi; naye Gabaeli akambariki Tobia na mkewe.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help