Ayubu UTANGULIZI - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

UTANGULIZIKitabu hiki ni kimojawapo cha vitabu viitwavyo “Maandiko ya Hekima”. Kimeandikwa kimashairi. Jina lake latokana na mtu ambaye habari zake zinasimuliwa kitabuni aitwaye Ayubu.Ayubu alikuwa mcha Mungu, mwenye heri, mali nyingi na hekima. Aliishi Usi iliyoko mashariki ya Palestina. Mwovu alidai kuwa mtu humwamini, humcha na humtegemea Mungu kwa sababu anaishi maisha ya heri. Kinyume chake angeliasi (1:9-11; 2:4-5). Mungu aliruhusu masaibu kwa Ayubu ili kupinga madai ya mwovu na kuthibitisha uthabiti wa imani ya Ayubu na kumtegemea Mungu (1:8; 2:3). Katika hali hiyo rafiki zake walimwendea wakidai kuwa maafa yake yalisababishwa na dhambi zake za sirini. Ayubu alifahamu kuwa hakuwa mkamilifu, lakini alikataa hoja za rafiki zake.Majadiliano kati ya Ayubu na rafiki zake ndiyo sehemu kubwa ya kitabu hiki. Kiini cha mazungumzo ni suala la kumcha Mungu, kuishi kwa uadilifu, maana ya maisha, mateso ya mwanadamu hapa duniani na Mungu anavyoangalia watu wake.Ayubu akiwa katika shida na machungu makali aliendelea katika imani na kumtegemea Mungu ijapokuwa mara kadhaa alimlalamikia Mungu. Mungu alitoa tamko lake kuhusu malalamiko hayo. Ayubu alikiri kuwa amesema bila kufikiri sawasawa maana Mungu ndiye mweza wa yote. Mwishoni Mungu akambariki Ayubu, akampa zaidi ya aliyokuwa nayo hapo awali na kuwakemea rafiki zake Ayubu.Yaliyomo:1. Utangulizi: Shetani amjaribu Ayubu, Sura 1–22. Ayubu ailaani siku ya kuzaliwa kwake, Sura 33. Sehemu tatu za mahojiano, Sura 4–274. Wimbo wa sifa za hekima, Sura 285. Hatima ya mahojiano, Sura 29–316. Hoja za Elihu, Sura 32–377. Hoja za Mungu, Sura 38–418. Maneno ya kufunga, Sura 42
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help