Zaburi 124 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Shukrani kwa ukombozi wa IsraeliWimbo wa kupanda mlima.

1 Mwa 15:1; Hes 14:9; Yos 1:5; Ebr 13:5; Rum 8:31 Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,

Israeli na aseme sasa,

2Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,

Wanadamu walipotushambulia.

3 Zab 35:25; Mit 1:12; Yer 51:34 Papo hapo wangalitumeza hai,

Hasira yao ilipowaka juu yetu.

4Papo hapo maji yangalitugharikisha,

Mto ungalipita juu ya roho zetu;

5Papo hapo maji yafurikayo

Yangalipita juu yetu.

6Na ahimidiwe BWANA;

Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.

7Nafsi yetu imeokoka kama ndege

Katika mtego wa wawindaji,

Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.

8 Kut 18:4; Zab 12:2; Mit 18:10; Isa 50:10; Ebr 13:6 Msaada wetu u katika jina la BWANA,

Aliyeziumba mbingu na nchi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help