Maombolezo 2 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Maonyo ya Mungu yatimizwa

1 Mt 11:23; 2 Sam 1:19; 1 Nya 28:2 Jinsi Bwana alivyomfunika binti Sayuni

Kwa wingu katika hasira yake!

Ameutupa toka mbinguni hata nchi

Huo uzuri wa Israeli;

Wala hakukikumbuka kiti cha miguu yake

Katika siku ya hasira yake.

2 Zab 89:39 Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo,

Wala hakuona huruma;

Ameziangusha ngome za binti Yuda

Katika ghadhabu yake;

Amezibomoa hata nchi

Ameunajisi ufalme na wakuu wake.

3 Ayu 16:15; Zab 74:11 Ameikata pembe yote ya Israeli

Katika hasira yake kali;

Ameurudisha nyuma mkono wake wa kulia

Mbele ya hao adui,

Naye amemteketeza Yakobo kama moto uwakao,

Ulao pande zote.

4 Isa 63:10 Ameupinda upinde wake kama adui,

Amesimama na mkono wake wa kulia kama mtesi;

Naye amewaua hao wote

Waliopendeza macho;

Katika hema ya binti Sayuni

Amemimina ghadhabu yake kama moto.

5 Yer 52:13 Bwana amekuwa mfano wa adui,

Amemmeza Israeli;

Ameyameza majumba yake yote,

Ameziharibu ngome zake;

Tena amemzidishia binti Yuda

Matanga na maombolezo.

6 Zab 80:12; Sef 3:18; Isa 5:5; 1:8 Naye ameondoa maskani yake kwa nguvu,

Kana kwamba ni ya bustani tu;

Ameziharibu sikukuu zake;

BWANA amezisahaulisha katika Sayuni

Sikukuu na sabato;

Naye amewadharau mfalme na kuhani

Katika uchungu wa hasira yake.

7 Zab 78:59-61; Eze 7:20; Isa 64:10,11; Mik 3:12; Yer 7:12-14; Mt 24:2; Zab 74:4 Bwana ameitupilia mbali madhabahu yake,

Amepachukia patakatifu pake;

Amezitia katika mikono ya hao adui

Kuta za majumba yake;

Wamepiga kelele ndani ya nyumba ya BWANA

Kama katika sikukuu.

8 Isa 34:11; Amo 7:7 BWANA amekusudia kuuharibu

Ukuta wa binti Sayuni;

Ameinyosha hiyo kamba,

Hakuuzuia mkono wake usiangamize;

Bali amefanya boma na ukuta kuomboleza;

Zote pamoja hudhoofika.

9 Kum 28:36; 2 Fal 25:7; 2 Nya 15:3; Zab 74:9; Amo 8:11,12; Mik 3:6,7 Malango yake yamezama katika nchi;

Ameyaharibu makomeo yake na kuyavunja;

Mfalme wake na wakuu wake wanakaa

Kati ya mataifa wasio na sheria;

Naam, manabii wake hawapati maono

Yatokayo kwa BWANA.

10 Ayu 2:13; Omb 4:5; Isa 47:1-5 Wazee wa binti Sayuni huketi chini,

Hunyamaza kimya;

Wametupa mavumbi juu ya vichwa vyao,

Wamejivika viunoni nguo za magunia;

Wanawali wa Yerusalemu huinama vichwa vyao

Kuielekea nchi.

11 Zab 6:7; Ayu 16:13 Macho yangu yamechoka kwa machozi,

Mtima wangu umetaabika;

Ini langu linamiminwa juu ya nchi

Kwa uharibifu wa binti ya watu wangu;

Kwa sababu watoto wachanga na wanyonyao,

Huzimia katika mitaa ya mji.

12Wao huwauliza mama zao,

Ziko wapi nafaka na divai?

Hapo wazimiapo kama waliojeruhiwa

Katika mitaa ya mji,

Hapo walipomiminika nafsi zao

Vifuani mwa mama zao.

13 Ayu 5:1; Dan 9:12 Nikushuhudie nini? Nikufananishe na nini,

Ee Binti Yerusalemu?

Nikulinganishe na nini, nipate kukufariji,

Ee bikira binti Sayuni?

Kwa maana uvunjifu wako ni mkuu kama bahari,

Ni nani awezaye kukuponya?

14 Isa 58:1 Manabii wako wameona maono kwa ajili yako

Ya ubatili na upumbavu

Wala hawakufunua uovu wako,

Wapate kurudisha kufungwa kwako;

Bali wameona mabashiri ya ubatili kwa ajili yako

Na sababu za kuhamishwa.

15 1 Fal 9:8; Zab 48:2 Hao watu wote wapitao

Hukupigia makofi;

Humzomea binti Yerusalemu,

Na kutikisa vichwa vyao;

Je! Mji huu ndio ulioitwa, Ukamilifu wa uzuri,

Furaha ya dunia yote?

16 Zab 56:2; 35:21 Juu yako adui zako wote

Wamepanua vinywa vyao;

Huzomea, husaga meno yao,

Husema, Tumemmeza;

Hakika siku hii ndiyo tuliyoitazamia;

Tumeipata, tumeiona.

17 Law 26:16; Zab 38:16; Kum 28:15,43,44; Omb 1:5 BWANA ameyatenda aliyoyakusudia; amelitimiza neno lake,

Aliloliamuru siku za kale;

Ameangusha hata chini,

Wala hakuona huruma;

Naye amemfurahisha adui juu yako,

Ameitukuza pembe ya watesi wako.

18 Yer 14:17; Omb 1:16 Mioyo yao ilimlilia Bwana;

Ee ukuta wa binti Sayuni!

Machozi na yachuruzike kama mto

Mchana na usiku;

Usijipatie kupumzika;

Mboni ya jicho lako isikome.

19 Mk 13:35; Zab 62:8; Isa 51:20; Omb 4:1; Nah 3:10 Inuka, ulalamike usiku,

Mwanzo wa mikesha yake;

Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana;

Umwinulie mikono yako;

Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa,

Mwanzo wa kila njia kuu.

20 Kut 32:11; Law 26:29; Kum 28:53; Yer 19:9; Omb 4:10,13 Tazama, BWANA, uangalie,

Ni nani uliyemtenda hayo!

Je! Wanawake wale mazao yao,

Watoto waliowabeba?

Je! Kuhani na nabii wauawe

Katika patakatifu pa Bwana?

21 2 Nya 36:17 Kijana na mzee hulala chini

Katika njia kuu;

Wasichana wangu na wavulana wangu

Wameanguka kwa upanga;

Umewaua katika siku ya hasira yako;

Umeua, wala hukuona huruma.

22 Zab 31:13; Yer 46:5; Hos 9:12 Umeziita kama katika siku ya mkutano wa makini;

Hofu zangu zije pande zote;

Wala hapana hata mmoja aliyepona wala kusalia

Katika siku ya hasira ya BWANA;

Hao niliowabeba na kuwalea

Huyo adui yangu amewakomesha.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help