1 Mambo ya Nyakati 22 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

1 nami nitawapa Israeli amani na utulivu siku zake;

102 Sam 7:13; 1 Fal 5:5; 1 Nya 17:12; 28:6; Zab 89:26,27; Ebr 1:5 huyo ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya jina langu; naye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa babaye; nami nitakiimarisha milele kiti cha ufalme wake juu ya Israeli.

11Rum 8:31 Sasa mwanangu, BWANA na awe pamoja nawe; ukafanikiwe, na kuijenga nyumba ya BWANA, Mungu wako, kama alivyonena kuhusu habari zako.

12Kum 4:6; 1 Fal 3:9; Zab 72:1 BWANA na akupe busara na akili, akakuagizie juu ya Israeli; ili uishike Torati ya BWANA, Mungu wako.

13Yos 1:7; 1 Fal 6:12,13; 9:4,5; 1 Nya 11:9,15; 28:7; Isa 3:10; Kum 31:7; 1 Nya 28:20 Ndipo utakapofanikiwa, ukiangalia kuzitenda amri, na hukumu, BWANA alizomwagizia Musa juu ya Israeli; uwe hodari, na wa moyo mkuu; usiogope wala usifadhaike.

14Basi sasa, tazama, katika shida yangu, nimeiwekea akiba nyumba ya BWANA, talanta laki moja za dhahabu, na talanta milioni moja za fedha; na shaba na chuma isiyo na uzani; kwa vile zilivyo tele; miti tena na mawe nimeweka akiba, nawe utaweza kuongeza.

15Tena kwako kuna mafundi wengi, wenye kuchonga na kufanya kazi ya mawe na miti, na kila aliye stadi kwa kazi yoyote;

16ya dhahabu, ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, hapana hesabu; basi inuka ushike kazi, naye BWANA na awe pamoja nawe.

17Tena Daudi akawaamuru viongozi wote wa Israeli, kwamba wamsaidie Sulemani mwanawe, akisema,

18Kum 12:10; Yos 22:4; 2 Sam 7:1; 1 Nya 23:25 Je! Si BWANA, Mungu wenu, aliye pamoja nanyi? Na kuwapa amani pande zote? Kwa kuwa wenyeji wa nchi amewatia mkononi mwangu; nayo nchi imetiishwa mbele za BWANA, na mbele ya watu wake.

192 Nya 20:3; 1 Fal 8:6; 2 Nya 5:7; 6:11 Basi sasa jitieni moyo na nia kumtafuta BWANA, Mungu wenu; inukeni basi, mkamjengee BWANA Mungu mahali patakatifu, ili kulileta sanduku la Agano la BWANA, na vyombo vitakatifu vya Mungu, ndani ya nyumba itakayojengwa kwa ajili ya jina la BWANA.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help