Ezra UTANGULIZI - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

UTANGULIZIEzra anayefikiriwa kuwa mwandishi wa Kitabu hiki alikuwa kuhani, mwandishi wa Mfalme Artashasta na mmoja wa viongozi wa Wayahudi waliporudi kutoka uhamishoni (7:11-12). Maana ya jina Ezra ni “msaada”. Ezra alitumia maandiko kadhaa ili kukamilisha kitabu hiki (1:2-4; 2:1-70; 4:7-22; 5:6-17; 6:3-12).Mwandishi anaanza kwa habari za tangazo rasmi la Mfalme Koreshi wa Persia, linaloruhusu Wayahudi kurejea makwao na kujenga upya hekalu la Yerusalemu (1:1-11). Wayahudi wengi walirudi Yuda wakaanza kujenga madhabahu na kufanya ibada kwa BWANA (2:1-70; 3:1-6), vile vile kuanzisha ujenzi wa hekalu. Kazi hii ilikumbana na upinzani mkubwa hata hivyo waliweza kumaliza ujenzi wa hekalu na kuta zake (3:7–6:22).Mfalme Artashasta wa Persia alimtuma kuhani Ezra kufufua, kusimamia na kurekebisha maisha ya kidini katika Yerusalemu. Naye Ezra alitekeleza agizo hilo. Kimsingi kitabu hiki kinaonesha maisha ya kidini na kijamii mjini Yerusalemu. Aidha mafanikio yalitokana na juhudi za makusudi katika kuitii sheria ya Mungu. Pale sheria ilipokuwa imevunjwa toba na marejeo vilifanywa na ilipokuwa imepuuzwa utii ulilazimishwa.Yaliyomo:1. Wayahudi kurudi toka uhamishoni, Sura 1–22. Ujenzi wa hekalu katika Yerusalemu, Sura 3–63. Kurudi kwake Ezra na matengenezo ya jumuiya, Sura 7–10
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help