Waraka kwa Waebrania 4 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Pumziko aliloahidi Mungu

1 Zab 95:11 Basi, ikiwa ingalipo ahadi ya kuingia katika pumziko lake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.

2Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa Habari Njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.

3Zab 95:11 Maana sisi tulioamini tunaingia katika pumziko lile; kama vile alivyosema,

Kama nilivyoapa kwa hasira yangu,

Hawataingia pumzikoni mwangu:

ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.

4Mwa 2:2 Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote;

5Zab 95:11 na tena kunena hapa napo, Hawataingia pumzikoni mwangu.

6Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,

7Zab 95:7-8 aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo, kama ilivyonenwa tangu zamani,

Leo, kama mkisikia sauti yake,

Msifanye mioyo yenu migumu.

8 Kum 31:7; Yos 22:4 Maana kama Yoshua angaliwapa pumziko, asingaliinena siku nyingine baadaye.

9Basi, limesalia pumziko la sabato kwa watu wa Mungu.

10Mwa 2:2; Ufu 14:13 Kwa maana yeye aliyeingia katika pumziko lake amepumzika mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyopumzika katika kazi zake.

11Basi, na tufanye bidii kuingia katika pumziko lile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka kwa mfano huo huo wa kuasi.

12Yer 23:29; Isa 49:2; Efe 6:17; Yn 12:48; Ufu 19:15 Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

13Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake.

Yesu aliye Kuhani Mkuu

14 Ebr 3:1; 6:20; 7:26; 8:1; 9:11 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.

15Ebr 2:17 Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuliana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa kama sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.

161 Yoh 3:21; Rum 3:25 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help