1Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha,
Mshangilieni Mungu wa Yakobo.
2Pazeni zaburi, pigeni matari,
Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda.
3 Hes 10:10 Pigeni panda mwandamo wa mwezi,
Kukiwa na mbalamwezi, wakati wa sikukuu yetu.
4 Law 23:24; Hes 10:10 Kwa maana ni sheria kwa Israeli,
Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo.
5Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu,
Alipoondoka juu ya nchi ya Misri;
Maneno yake nisiyemjua niliyasikia.
6Nimeutua mzigo begani mwake;
Mikono yake nikaiondolea kazi nzito.
7 Kut 17:7; Hes 20:13 Katika shida uliniita nikakuokoa;
Nilikuitikia kutoka maficho yangu ya radi;
Nilikujaribu penye maji ya Meriba.
8Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya,
Ee Israeli, kama ukitaka kunisikiliza;
9 Kut 20:2-3; Kum 5:6-7 Usiwe na mungu mgeni ndani yako;
Wala usimsujudie mungu mwingine.
10 Zab 37:3; Yn 15:7 Mimi ndimi BWANA, Mungu wako,
Niliyekupandisha toka nchi ya Misri;
Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.
11Lakini watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu,
Wala Israeli hawakunitaka.
12 Mdo 7:42; Rum 1:24 Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao,
Waenende katika mashauri yao.
13 Kum 5:29; Isa 48:18; Yer 44:4,5; Mt 23:37 Laiti watu wangu wangenisikiliza,
Na Israeli angeenenda katika njia zangu;
14Ningewadhili adui zao kwa upesi,
Na juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu;
15Wamchukiao BWANA wangenyenyekea mbele zake,
Na maangamizi yao yangedumu milele.
16Naam, ningewalisha kwa ngano iliyo bora zaidi,
Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.