Hesabu 34 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Mipaka ya nchi

1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

2 upande wa mashariki;

12kisha mpaka utateremkia Yordani, na kutokea kwake kutakuwa hapo katika Bahari ya Chumvi; hii ndiyo nchi yenu kama mipaka yake ilivyo kuizunguka pande zote.

13Hes 26:52-56; Yos 14:1,2 Kisha Musa akawaagiza wana wa Israeli, akisema, Hii ndiyo nchi mtakayoirithi kwa kupiga kura, ambayo BWANA ameagiza wapewe watu wa yale makabila tisa, na nusu ya kabila;Yos 14:1-5

14Hes 32:33; Yos 14:2,3 kwa kuwa kabila la wana wa Reubeni kwa nyumba za baba zao, na kabila la wana wa Gadi kwa nyumba za baba zao, wamekwisha pata, na hiyo nusu ya kabila la Manase wamekwisha pata urithi wao;

15hayo makabila mawili na nusu ya kabila wamekwisha pata urithi wao huko ng'ambo ya pili ya Yordani, hapo Yeriko, upande wa mashariki, kuelekea mawio ya jua.

Viongozi wa makabila

16Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

17Kut 6:23-25 Haya ndiyo majina ya watu watakaowagawanyia nchi iwe urithi wenu; Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni.

18Kisha mtamtwaa mkuu mmoja wa kila kabila, ili waigawanye nchi iwe urithi wenu.

19Mwa 29:35; 49:8-10; Kum 33:7; Zab 60:7; 108:8; Hes 13:6,30; Kum 1:36 Na majina ya watu hao ni haya; katika kabila la Yuda, ni Kalebu mwana wa Yefune.

20Mwa 29:33; 49:5; Eze 48:24 Na katika kabila la wana wa Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.

21Mwa 35:18; 49:27; Kum 33:12; Zab 68:27; 80:2 Katika kabila la Benyamini, ni Elidadi mwana wa Kisloni.

22Na katika kabila la wana wa Dani, mkuu, Buki mwana wa Yogli.

23Mwa 48:8-22; 49:22; Kum 33:13; Zab 80:1 Katika wana wa Yusufu; katika kabila la wana wa Manase, mkuu, Hanieli mwana wa Efodi;

24na katika kabila la wana wa Efraimu, mkuu, Kemueli mwana wa Shiftani.

25Na katika kabila la wana wa Zabuloni, mkuu, Elisafani mwana wa Parnaki.

26Na katika kabila la wana wa Isakari, mkuu, Paltieli mwana wa Azani.

27Na katika kabila la wana wa Asheri, mkuu, Ahihudi mwana wa Shelomi.

28Na katika kabila la wana wa Naftali, mkuu, Pedaheli mwana wa Amihudi.

29Kum 32:8; Mdo 17:26 Hao ndio BWANA aliowaagiza wawagawanyie urithi wana wa Israeli katika nchi ya Kanaani.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help