1 Isa 2:11; Zek 14:20,21 Na katika siku hiyo utasema,
Ee BWANA, nitakushukuru wewe;
Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia,
Hasira yako imegeukia mbali,
Nawe unanifariji moyo.
2 Kut 15:2; Zab 118:14 Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;
Nitatumaini wala sitaogopa;
Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu;
Naye amekuwa wokovu wangu.
3 Yer 2:13; Yn 4:10,14 Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.
4Na katika siku hiyo mtasema,
Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake;
Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa,
Litangazeni jina lake kuwa limetukuka.
5Mwimbieni BWANA; kwa kuwa ametenda makuu;
Na yajulikane haya katika dunia yote.
6 Isa 54:1; Sef 3:14; Lk 19:37-40 Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;
Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.