Zaburi 1 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

KITABU CHA KWANZANjia mbili

1 Mwa 5:24; Ayu 31:5; Zab 81:12; Mit 4:14 Heri mtu yule asiyekwenda

Katika shauri la wasio haki;

Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi;

Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

2Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,

Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

3 Yer 17:8; Mwa 39:3; Zab 128:2 Naye atakuwa kama mti uliopandwa

Kandokando ya vijito vya maji,

Uzaao matunda yake kwa majira yake,

Wala jani lake halinyauki;

Na kila alitendalo litafanikiwa.

4Sivyo walivyo wasio haki;

Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

5Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni,

Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.

6 Nah 1:7; Yn 10:14 Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki,

Bali njia ya wasio haki itapotea.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help