Luka 22 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Mpango wa kumwua Yesu

1

40Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni.

41Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba,

42Mt 6:10 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; lakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.

45Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala usingizi kwa huzuni.

46Akawaambia, Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni.

Kusalitiwa na kukamatwa kwa Yesu

47 Mt 26:47-56; Mk 14:43-49; Yn 18:2-11 Basi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Kumi na Wawili, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu.

48Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu?

49Na wale waliokuwa karibu naye walipoona yatakayotokea, walisema, Bwana, tuwapige kwa upanga?

50Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kulia.

51Yesu akajibu akasema, Muwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio, akamponya.

52Lk 22:37 Yesu akawaambia wakuu wa makuhani, na maofisa wa hekalu, na wazee, waliokuja juu yake, Je! Mmekuja mkiwa na panga na marungu kama kukamata mnyang'anyi?

53Lk 19:47; 21:37; Yn 7:30; 8:20; Kol 1:13 Kila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono, lakini hii ndiyo saa yenu, ya mamlaka ya giza.

Petro amkana Yesu

54 Mt 26:57,58,69-75; Mk 14:53,54,66-72; Yn 18:12-18,25-27 Wakamkamata, wakamchukua, wakaenda naye nyumbani kwa Kuhani Mkuu. Na Petro alimfuata kwa mbali.

55Na walipokwisha washa moto katikati ya kiwanja, waliketi pamoja, naye Petro akaketi kati yao.

56Ndipo mjakazi mmoja akamwona ameketi akiwa katika mwanga, akamkazia macho akasema, Na huyu alikuwa pamoja naye.

57Akakana, akisema, Ee mwanamke, simjui.

58Muda mfupi baadaye mtu mwingine alimwona akasema, Wewe nawe u mmoja wao. Petro akasema, Ee mtu, si mimi.

59Halafu, yapata saa moja, mtu mwingine alikazia akisema, Hakika na huyu alikuwa pamoja naye, kwa kuwa yeye pia ni Mgalilaya.

60Petro akasema, Ee mtu, sijui usemalo. Na papo hapo alipokuwa katika kusema, jogoo aliwika.

61Lk 22:34 Bwana akageuka akamtazama Petro. Petro akalikumbuka lile neno la Bwana jinsi alivyomwambia, Leo kabla hajawika jogoo utanikana mara tatu.

62Akatoka nje akalia kwa majonzi.

Kumdhihaki na kumpiga Yesu

63 Mt 26:67,68; Mk 14:65 Na wale watu waliokuwa wakimshika Yesu walimfanyia dhihaka, wakampiga.

64Wakamfunika macho, kisha wakamwulizauliza wakisema, Tabiri, ni nani aliyekupiga?

65Wakamtolea na maneno mengine mengi ya kumtukana.

Yesu mbele ya baraza

66 Mt 26:59-66; Mk 14:55-64 Kulipokucha, walikutanika jamii ya wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, wakamleta katika baraza yao, wakisema,

67Yn 3:12; 8:45; 10:24 Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie. Akawaambia, Nikiwaambia, hamtasadiki.

68Tena, nikiwauliza, hamtajibu.

69Dan 7:13; Zab 110:1 Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi.

70Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.

71Wakasema, Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? Maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help