Mwanzo 20 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Abrahamu na Sara wakiwa Gerari

1 Mwa 18:1; 26:6 Abrahamu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari.

2Mwa 12:11-15; 26:7 Abrahamu akanena juu ya Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu”. Basi Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma watu wakamtwaa Sara.

3Zab 105:14; Ayu 4:12; 33:15; Mwa 19:7 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mke wa mtu.

4Mwa 18:23-25 Basi Abimeleki alikuwa hakumkaribia, akasema, Ee Bwana, Je! Utaua hata taifa lenye haki?

5Je! Hukuniambia mwenyewe, “Huyu ni dada yangu?” Na mwanamke mwenyewe naye akasema, “Huyu ni kaka yangu”. Kwa ukamilifu wa moyo wangu, na kwa kutojua kwangu, nimefanya hivi.

6Mwa 35:5; Kut 34:4; 1 Sam 25:26,34 Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse.

71 Sam 7:5; 2 Fal 5:11; Ayu 42:8; Yak 5:14-16; 1 Yoh 5:16 Basi sasa umrudishe mwanamke kwa mtu huyo, maana yeye ni nabii, naye atakuombea, upate kuishi. Bali usipomrudisha, fahamu ya kwamba kwa hakika utakufa wewe na watu wote ulio nao.

8Abimeleki akaamka asubuhi na mapema, akawaita watumwa wake wote, akawaambia maneno hayo yote, nao watu hao wakaogopa sana.

9Mwa 39:9; Yos 7:25 Kisha Abimeleki akamwita Abrahamu, akamwambia, Umetutenda nini? Nimekukosa nini, hata ukaleta juu yangu na juu ya ufalme wangu dhambi kuu? Umenitenda matendo yasiyotendeka.

10Abimeleki akamwambia Abrahamu, Umeona nini hata ukatenda jambo hili?

11Mwa 42:18; Neh 5:15; Mit 16:6 Abrahamu akasema, Kwa kuwa niliona, hakika hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua kwa ajili ya mke wangu.

12Mwa 11:29 Hata hivyo, kwa kweli yeye ni dada yangu, yaani binti wa baba yangu na wala sio binti wa mama yangu; ndipo akawa mke wangu.

13Mwa 12:1,9,10,13 Ikawa hapo Mungu aliponisafirisha kutoka nyumba ya baba yangu, nikamwambia, Hii ndiyo fadhili yako, utakayonifanyia. Kila mahali tuingiapo, useme, Huyu ni kaka yangu.

14Mwa 12:16 Basi Abimeleki akatwaa kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi, akampa Abrahamu, akamrudishia Sara mkewe.

15 Mwa 13:9; 47:6 Abimeleki akasema, Nchi yangu iko mbele yako, ishi upendapo.

16Mwa 20:5 Naye akamwambia Sara, Tazama! Nimempa ndugu yako fedha elfu moja, itakuwa kifunika macho kwako mbele ya wote walio pamoja nawe, nawe utakuwa na haki mbele ya watu wote.

17Ayu 42:8; Yak 5:16 Abrahamu akamwomba Mungu, Mungu akamponya Abimeleki, na mkewe, na wajakazi wake, nao wakazaa wana.

18Mwa 12:17 Maana BWANA alikuwa ameyafunga matumbo ya watu wa nyumbani mwa Abimeleki, wasizae, kwa ajili ya Sara mkewe Abrahamu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help