Kutoka 40 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Hema lasimikwa na vifaa vyake kuwekwa wakfu

1BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

2Kut 12:2; 13:4; 25:9; 26:1,30; Hes 7:1; Mdo 7:44,45; Ebr 8:2-5; 9:2,11; Ufu 21:3 Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza utaisimamisha hiyo maskani ya hema ya kukutania.

3Hes 4:5 Nawe utatia ndani yake sanduku la ushuhuda, nawe utalisitiri hilo sanduku kwa pazia.

4Kut 26:35; Law 24:5,6 Nawe utaleta meza na kuitia ndani, na kuviweka sawasawa vile vitu juu yake; kisha utakileta ndani kile kinara cha taa, na kuziwasha taa zake.

5Ebr 9:24; 10:19-22 Kisha utaisimamisha madhabahu ya dhahabu kwa kufukizia uvumba mbele ya sanduku la ushuhuda, na kulitia pazia mlangoni mwa hiyo maskani.

6Kisha utaweka madhabahu ya kuteketeza sadaka mbele ya mlango wa maskani ya hema ya kukutania.

7Kut 30:18 Kisha utaliweka birika kati ya hema ya kukutania na hiyo madhabahu, nawe utatia maji ndani yake.

8Kisha utausimamisha ukuta wa ua kuuzunguka pande zote, na kuitundika sitara ya lango la ua.

9Kut 30:23-26 Kisha utayatwaa mafuta ya kutiwa, na kuitia mafuta hiyo maskani, na kila kitu kilicho ndani yake, na kuiweka iwe takatifu, na vyombo vyake vyote; nayo itakuwa takatifu.

10Kut 29:36 Kisha utaitia mafuta madhabahu ya kuteketeza sadaka, na vyombo vyake vyote; na kuiweka takatifu madhabahu; na hiyo madhabahu itakuwa takatifu sana.

11Kisha utalitia mafuta birika na kitako chake, na kuliweka liwe takatifu.

12 Law 8:1-13 Kisha utamleta Haruni na wanawe hapo mlangoni pa hema ya kukutania, nawe utawaosha kwa maji.

13Kut 28:41; Zab 133:2 Kisha utamvika Haruni mavazi matakatifu; nawe utamtia mafuta, na kumweka awe mtakatifu, ili apate kunitumikia katika kazi ya ukuhani.

14Ebr 7:23 Kisha utawaleta wanawe, na kuwavika kanzu zao;

15Hes 25:13; Ebr 7:11; Ufu 1:6; 1 Pet 2:5,9 nawe utawatia mafuta kama ulivyomtia mafuta baba yao, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani; na huko kutiwa mafuta kwao kutakuwa ni kwa ukuhani wa milele katika vizazi vyao vyote.

16Musa akafanya hayo yote; kama BWANA aliyoagiza ndivyo alivyofanya yote.

17 Hes 7:1 Hata mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili, siku ya kwanza ya mwezi maskani ile ilisimamishwa.

18Musa akaisimamisha maskani, akaviweka vitako vyake, akazisimamisha mbao zake akayatia mataruma yake, akazisimamisha nguzo zake.

19Akaitanda hema juu ya maskani, akakitia kifuniko cha hema juu yake; kama BWANA alivyomwamuru Musa.

20Kut 25:16; Zab 78:5; Isa 8:20 Akautwaa ule ushuhuda, akautia ndani ya sanduku, akaiweka miti ya kuchukulia juu ya sanduku, akakiweka kiti cha rehema juu ya sanduku;

21Kut 35:12 kisha akalileta sanduku akalitia ndani ya maskani, naye akalitundika pazia la sitara, akalisitiri sanduku la ushuhuda; kama BWANA alivyomwamuru Musa.

22Kut 26:35 Akaitia meza ndani ya hema ya kukutania, upande wa maskani ulioelekea kaskazini, nje ya pazia.

23Akaipanga ile mikate juu yake mbele za BWANA; kama BWANA alivyomwamuru Musa.

24Kut 26:35 Kisha akakitia kinara cha taa ndani ya hema ya kukutania, kuikabili ile meza, upande wa maskani ulioelekea kusini.

25Kut 25:37 Kisha akaziwasha taa zake mbele za BWANA, kama BWANA alivyomwamuru Musa.

26Kut 30:6 Akaitia madhabahu ya dhahabu ndani ya hema ya kukutania mbele ya pazia.

27Kut 30:7 Akafukiza juu yake uvumba wa manukato kama BWANA alivyomwamuru Musa.

28Kut 26:36 Akalitia pazia la mlango wa maskani.

29Kut 29:38 Akaiweka madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mlangoni pa maskani ya kukutania, akatoa sadaka ya kuteketezwa juu yake, na sadaka ya unga; kama BWANA alivyomwamuru Musa.

30Kut 30:18 Akaliweka birika kati ya hema ya kukutania na madhabahu, akatia maji ndani yake ya kuoshea.

31Musa na Haruni, na wanawe wakanawa mikono yao na miguu yao ndani yake;

32Kut 30:19 hapo walipoingia hema ya kukutania, na hapo walipoikaribia madhabahu walinawa kama BWANA alivyomwamuru Musa.

33Kut 27:9,16 Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi.

Wingu na utukufu wa BWANA

34 1 Fal 8:10-11; Isa 6:4; Eze 43:4-5; Ufu 15:8; Law 16:2; Hes 9:15; 2 Nya 5:13; 7:2; Hag 2:7,9 Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.

351 Fal 8:11; 2 Nya 5:14; Zab 78:14 Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania, kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.

36Hes 10:11; Neh 9:19 Na hapo lile wingu lilipoinuliwa kutoka juu ya maskani, wana wa Israeli wakaenda mbele katika safari zao zote,

37Hes 9:19-22 bali kama lile wingu halikuinuliwa, wakati ule hawakusafiri hadi siku ile lilipoinuliwa tena.

38Kut 13:21; Hes 9:15 Kwa maana lile wingu la BWANA lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana, na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku, mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safari zao zote.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help