Ayubu 23 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Ayubu ajibu: Malalamiko yangu ni machungu

1Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,

2Hata leo malalamiko yangu yana uchungu;

Pigo langu ni zito zaidi ya kuugua kwangu.

3Laiti ningejua mahali niwezapo kumwona,

Nifike hata hapo anapokaa!

4Ningeiweka kesi yangu mbele yake,

Na kukijaza kinywa changu hoja.

5Ningeyajua maneno atakayonijibu,

Na kuelewa hayo atakayoniambia.

6 Ayu 9:19; Isa 27:4 Je! Angeshindana nami kwa ukuu wa uwezo wake?

La, lakini angenisikiliza.

7Hapo wanyofu wangepata kuhojiana naye;

Basi hivyo ningeachiliwa na mwamuzi wangu milele.

8 Zab 10:1; 1 Tim 6:16 Tazama, naenda mbele, wala hayuko;

Narudi nyuma, lakini siwezi kumwona;

9Na mkono wa kushoto, afanyapo kazi, lakini siwezi kumwona;

Hujificha upande wa kulia, hata nisimwone.

10 Zab 17:3; Yak 1:12 Lakini yeye aijua njia niendeayo;

Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.

11 Zab 44:18 Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake;

Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.

12Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake;

Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu,

13 Ayu 34:29; Mhu 3:14; Rum 9:19; Yak 1:17 Lakini yeye ni mmoja, ni nani awezaye kumgeuza?

Tena nafsi yake ilitakalo, ndilo afanyalo.

14 1 The 3:3 Kwani yeye hulitimiliza hilo nililoamriwa;

Tena mambo mengi kama hayo ya pamoja naye.

15 Zab 119:120 Kwa hiyo naona taabu mbele ya uso wake;

Nitakapofikiri, namwogopa.

16Kwa maana Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia,

Naye Mwenyezi amenitaabisha;

17 Ayu 6:9 Maana sikufadhaishwa kwa sababu ya giza,

Wala kwa sababu giza kuu limenifunika uso.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help