1
Na mafuta mifupani mwako.
9 Kut 23:19 Mheshimu BWANA kwa mali yako,
Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
10 Kum 28:8 Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi,
Na vyombo vyako vitafurika divai mpya.
11 Ayu 5:17; Ebr 12:5 Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na BWANA,
Wala usione ni taabu kurudiwa naye.
12 Ufu 3:19; Kum 8:5 Kwa kuwa BWANA ampendaye humrudi,
Kama vile baba mwanawe ampendezaye.
Utajiri wa kweli13Heri mtu yule aonaye hekima,
Na mtu yule apataye ufahamu.
14 Ayu 28:13; Mit 2:4; 8:11,19 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha,
Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.
15 Mt 13:44 Yeye ana thamani kuliko marijani,
Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.
16 1 Tim 4:8 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kulia,
Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.
17 Mt 11:29 Njia zake ni njia za kupendeza sana,
Na mapito yake yote ni amani.
18 Mwa 2:9 Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana;
Ana heri kila mtu anayeshikamana naye.
Hekima ya Mungu katika uumbaji19 Mit 8:27; Yn 1:3; Ebr 1:2 Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi;
Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;
20 Kum 33:28; Ayu 36:28 Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika;
Na mawingu yadondoza umande.
Usalama wa kweli21Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako,
Shika hekima kamili na busara.
22Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako,
Na neema shingoni mwako.
23Ndipo utakapokwenda katika njia yako salama,
Wala mguu wako hautakwaa.
24 Law 26:6 Ulalapo hutaona hofu;
Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu.
25Usiogope hofu ya ghafla,
Wala uharibifu wa waovu utakapofika.
26Kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako,
Naye atakulinda mguu wako usinaswe.
27 Rum 13:7; Gal 6:10 Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao,
Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.
28 Law 19:13; Kum 24:15 Usimwambie jirani yako,
Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa;
Nawe unacho kitu kile karibu nawe.
29Usiwaze mabaya juu ya jirani yako,
Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama.
30 Rum 12:18 Usishindane na mtu bila sababu,
Ikiwa hakukudhuru kwa lolote.
31Usimhusudu mtu mwenye ujeuri,
Wala usiichague mojawapo ya njia zake.
32Maana mtu mjeuri ni chukizo kwa BWANA,
Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.
33 Zek 5:4; Mal 2:2; Zab 1:3 Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu,
Bali huibariki maskani ya mwenye haki.
34 Yak 4:6; 1 Pet 5:5; Zab 138:6; Mt 23:12 Hakika yake huwadharau wenye dharau,
Bali huwapa wanyenyekevu neema.
35 Dan 12:2 Wenye hekima wataurithi utukufu,
Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.