1Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu
Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu nitakayemtumaini.
3Maana Yeye atakuokoa kutoka kwenye mtego wa mwindaji,
Na katika maradhi mabaya.
4 Zab 61:4 Kwa manyoya yake atakufunika,
Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;
Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Ayu 5:19; Mit 3:23; Isa 43:2 Hutaogopa hatari za usiku,
Wala mshale urukao mchana,
6Wala mapigo yajayo usiku,
Wala maafa yatokeayo adhuhuri,
7Hata watu elfu wakianguka ubavuni pako.
Naam, watu elfu kumi katika mkono wako wa kulia!
Wewe hutakaribiwa na maafa.
8 Mal 1:5 Ila kwa macho yako utatazama,
Na kuyaona malipo ya wasio haki.
9Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu;
Umemfanya Aliye Juu kuwa makao yako.
10 Mit 1:33; 2 The 3:3; 2 Pet 2:9 Mabaya hayatakupata wewe,
Wala tauni haitaikaribia hema yako.
11 Mt 4:6; Lk 4:10; Zab 34:7; Ebr 1:14 Kwa kuwa atakuagizia malaika wake
Wakulinde katika njia zako zote.
12 Ayu 5:23; Zab 37:24; Mt 4:6; Lk 4:11 Mikononi mwao watakuchukua,
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13 Lk 10:19 Utawakanyaga simba na nyoka,
Mwanasimba na joka utawakanyaga kwa miguu.
14Kwa kuwa amekaza kunipenda
Nitamwokoa; na kumweka palipo juu,
Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15 Ayu 22:27; Zab 18:3; Yer 33:3; Zek 13:9; Ebr 5:7; Zab 43:2; 1 Sam 2:30 Ataniita nami nitamwitikia;
Nitakuwa pamoja naye taabuni,
Nitamwokoa na kumtukuza;
16Kwa siku nyingi nitamshibisha,
Nami nitamwonesha wokovu wangu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.