Isaya 33 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Unabii wa kukombolewa kutoka kwa watesi

1 kila asubuhi, na wokovu wetu pia wakati wa taabu.

3Makabila ya watu wamekimbia wakisikia kelele za fujo; mataifa wametawanyika ulipojiinua nafsi yako.

4Na mateka yako yatakusanywa kama wadudu wakumbavyo, wataruka juu yake kama arukavyo nzige.

5Zab 97:9 BWANA ametukuka; kwa maana anakaa juu; amejaza Sayuni hukumu na haki.

6Mit 1:7; Mt 6:33 Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba.

7 2 Fal 18:18 Angalia, mashujaa wao wanalia nje, wajumbe wa amani wanalia kwa uchungu.

8Amu 5:6; 2 Fal 18:14 Njia kuu zimeachwa, msafiri ameikimbia barabara; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu.

9Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani.

10Kum 32:36,43; Zab 12:5; Isa 42:13,14; Sef 3:8 Basi, sasa nitasimama; asema BWANA; sasa nitajiinua, sasa nitajitukuza.

11Ninyi mtachukua mimba ya makapi, mtazaa majani makavu; pumzi yenu ni moto utakaowateketeza wenyewe.

12Nao mataifa watakuwa kama kuchoma chokaa, kama miiba iliyokatika, iteketezwayo motoni.

13Sikieni, ninyi mlio mbali, niliyoyatenda; na ninyi mlio karibu, kirini uwezo wangu.

14Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uangamizao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?

15Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung'utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za umwagaji wa damu; afumbaye macho yake asitazame uovu.

16Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.

Nchi ya mfalme mkuu

17Macho yako yatamwona mfalme katika uzuri wake, yataona nchi iliyoenea sana.

181 Kor 1:20 Moyo wako utatafakari hofu ile; Yuko wapi yeye aliyehesabu? Yuko wapi yeye aliyeupima ushuru? Yuko wapi yeye aliyeihesabu minara?

19Yer 5:15 Hutawaona watu wale wakali; watu wa maneno magumu usiyoweza kuyafahamu; wenye lugha ya kigeni usiyoweza kuielewa.

20Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa makao ya raha; hema isiyotikisika; vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika.

21Zek 2:5 Bali huko BWANA atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito, pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo.

22Zab 44:4; Mt 21:5; Ufu 19:16 Kwa maana BWANA ndiye mwamuzi wetu; BWANA ndiye mfanya sheria wetu; BWANA ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.

23Kamba zako zimelegea; hawakuweza kukaza sana shina la mlingoti wao; hawakuweza kulikunjua tanga; ndipo mapato ya mateka yaligawanywa, hata wachechemeao walipata mateka.

24Isa 12:2; Rum 11:27 Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help