3Yohana 1 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Salamu

1 Mdo 19:29; Rum 16:23; 1 Kor 1:14; 2 Yoh 1:1 Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.

Gayo apongezwa kwa ukarimu wake

2 2 Yoh 1:4 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

3Maana nilifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli.

4Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.

5Mpenzi, kazi ile ni ya uaminifu uwatendeayo hao ndugu na hao wageni nao,

6Tit 3:13 waliokushuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kama ipasavyo kwa Mungu.

7Mdo 20:35; 1 Kor 9:12,15 Kwa maana, kwa ajili ya Jina hilo, walitoka, wasipokee kitu kwa Mataifa.

8Ebr 13:2; 2 Yoh 1:10 Basi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hao, ili tuwe watenda kazi pamoja na kweli.

Diotrefe na Demetrio

9Nililiandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali.

10Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.

Salamu za mwisho

11 1 Yoh 3:6,9 Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.

12Yn 19:35; 21:24 Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Nasi pia tunashuhudia, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli.

13 2 Yoh 1:12 Nilikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu.

14Lakini natarajia kukuona karibuni, nasi tutasema uso kwa uso.

15Amani kwako. Rafiki zetu wakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu, kila mtu kwa jina lake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help