1 Wakorintho 13 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Karama ya upendo

1Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

2Mt 17:20; 7:22; 21:21; Mk 11:23 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu.

3Mt 6:2 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidi kitu.

4Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

5Zek 8:17; Flp 2:4 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

6Rum 12:9 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

7Mit 10:12; 1 Kor 9:12; Rum 15:1 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

81 Pet 4:8 Upendo haupungui neno wakati wowote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.

9Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;

10lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.

11Nilipokuwa mtoto mchanga, nilisema kama mtoto mchanga, nilifahamu kama mtoto mchanga, nilifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.

122 Kor 5:7; Yak 1:23 Maana sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.

131 The 1:3; 1 Yoh 4:16 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help