Zaburi 142 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Sala ya ukombozi kutoka kwa watesiUtenzi wa Daudi. Alipokuwa pangoni. Ombi.

1 1 Sam 22:1; 24:3 Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA,

Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua.

2Nitafunua mbele zake malalamiko yangu,

Shida yangu nitaitangaza mbele zake.

3Roho yangu inapozimia unayajua mapito yangu;

Katika njia niendayo wamenifichia mtego.

4Utazame mkono wangu wa kuume ukaone,

Kwa maana sina mtu anijuaye.

Makimbilio yamenipotea,

Hakuna wa kunitunza roho.

5 Omb 3:24 BWANA, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu,

Fungu langu katika nchi ya walio hai.

6 Zab 116:6; 7:1 Ukisikilize kilio changu,

Kwa maana nimedhilika sana.

Uniponye kutoka kwao wanaonifuatia,

Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.

7 Zab 34:2; 119:17 Uitoe nafsi yangu kifungoni.

Nipate kulishukuru jina lako.

Wenye haki watanizunguka,

Kwa kuwa Wewe unanikirimu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help