1Haleluya.
Msifuni Bwana;
Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu sifa,
Maana ni mwenye fadhili, na anastahili kuimbiwa sifa.
2
11BWANA huwaridhia wao wamchao,
Na kuzitarajia fadhili zake.
12Msifu BWANA, Ee Yerusalemu;
Msifu Mungu wako, Ee Sayuni.
13Maana amevikaza vipingo vya malango yako,
Amewabariki wanao ndani yako.
14Ndiye aletaye amani mipakani mwako,
Hukushibisha kwa ngano safi.
15 Ayu 37:12 Huipeleka amri yake juu ya nchi,
Neno lake lapiga mbio sana.
16Ndiye atoaye theluji kama sufu,
Huimwaga barafu yake kama majivu,
17Hutupa mvua ya mawe kama makombo,
Mbele ya baridi yake ni nani awezaye kusimama?
18Hulituma neno lake na kuviyeyusha,
Huuvumisha upepo wake, maji yakatiririka.
19 Kum 33:4; Mal 4:4; Rum 3:2 Hulitangaza neno lake kwa Yakobo,
Na amri zake na hukumu zake kwa Israeli.
20 Kum 4:32; Mdo 14:16; Rum 3:1-2 Hakulitendea taifa lolote mambo kama hayo,
Wala hukumu zake hawakuzijua.
Haleluya.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.