1Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe,
Na kwa uweza wako unifanyie hukumu.
2Ee Mungu, uyasikie maombi yangu,
Uyasikilize maneno ya kinywa changu.
3Kwa maana wageni wamenishambulia;
Watu watishao wananitafuta nafsi yangu;
Hawakumweka Mungu mbele yao.
4 Zab 118:7; Isa 41:10; Rum 8:31,32; Ebr 13:6 Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia;
Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.
5 Zab 89:49 Atawarudishia adui zangu ubaya wao;
Uwaangamize kwa uaminifu wako.
6Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu;
Ee BWANA, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.
7Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu;
Na jicho langu limeridhika
Kwa kuwatazama adui zangu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.