Zaburi 11 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Wimbo wa kumtumainia MunguKwa mwimbishaji. Ya Daudi.

1BWANA ndiye niliyemkimbilia.

Mbona mnaiambia nafsi yangu,

Kimbia kama ndege mlimani kwenu?

2Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta,

Wanaitia mishale yao katika uta,

Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.

3Kama misingi ikiharibika,

Mwenye haki atafanya nini?

4 Hab 2:20; Efe 5:13; Ebr 4:13 BWANA yu katika hekalu lake takatifu.

BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni,

Macho yake yanaangalia;

Kope zake zinawapima wanadamu.

5 Ayu 5:17; Zab 94:12 BWANA humjaribu mwenye haki;

Bali nafsi yake humchukia asiye haki,

Na mwenye kupenda udhalimu.

6Awanyeshee wasio haki mitego,

Moto na kiberiti na upepo wa joto

Na viwe fungu la kikombe chao.

7Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki,

Apenda matendo ya haki,

Wanyofu wa moyo watauona uso wake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help