Hesabu 21 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Nyoka ya shaba

1

4Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia.

5 kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa.

7 utokao katika mpaka wa Waamori; maana, Arnoni ndio mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori.

14Kwa hiyo imesemwa katika Kitabu cha Vita vya BWANA,

Wahebu katika Sufa,

Na bonde za Arnoni,

15Na materemko ya hizo bonde

Kwenye kuteremkia maskani ya Ari,

Na kutegemea mpaka wa Moabu.

16 ni kisima ambacho BWANA alimwambia Musa, Uwakutanishe watu, nami nitawapa maji.

17 Kut 15:1; Zab 105:2 Ndipo Israeli wakaimba wimbo huu;

Bubujika Ee kisima; kiimbieni;

18 Kum 33:4; Isa 33:22 Kisima walichokichimba wakuu,

Ambacho wakuu wa watu wakakifukua,

Kwa fimbo za enzi, kwa fimbo zao.

Kutoka lile jangwa wakaenda Matana;

19na kutoka Matana wakaenda Nahalieli; na kutoka Nahalieli wakaenda Bamothi;

20Hes 23:28 na kutoka Bamothi wakaenda bondeni kwenye konde la Moabu, hata kilele cha Pisga, kielekeacho chini jangwani.

Kushindwa kwa mfalme wa Sihoni vitani

21 Kum 2:26; Amu 11:19 Kisha Israeli akatuma wajumbe kumwendea Sihoni mfalme wa Waamori, na kusema,

22Hes 20:17 Nipe ruhusa nipite katika nchi yako; hatutageuka kando kwenda mashambani, wala kuingia katika mashamba ya mizabibu hatutakunywa maji ya visimani; tutakwenda kwa njia kuu ya mfalme, hadi tutakapokuwa tumetoka katika mpaka wa nchi yako.

23Kum 29:7; 2:32,33 Lakini Sihoni hakukubali kumwacha Israeli kupita katika mpaka wake; bali Sihoni akawakutanisha watu wake wote, akatoka aende kupigana na Israeli jangwani, akafika mpaka Yahasa; akapigana na Israeli.

24Kum 29:7; Yos 12:1,2; 24:8; Neh 9:22; Zab 135:10; 136:19; Amo 2:9 Israeli wakampiga kwa makali ya upanga, na kuimiliki nchi yake, tangu mto wa Arnoni hata mto wa Yaboki, mpaka nchi ya wana wa Amoni; kwa kuwa mpaka wa wana wa Amoni ulikuwa una nguvu.

25Basi Israeli wakaitwaa miji hiyo yote; Israeli wakakaa katika miji yote ya Waamori, katika Heshboni, na miji yake yote.

26Kwa kuwa Heshboni ulikuwa ni mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akipigana na mfalme wa Moabu wa mbele, na kumpokonya nchi yake yote mkononi mwake, mpaka mto wa Arnoni.

27Kwa hiyo, hao wanenao kwa mithali wasema,

Njoni Heshboni,

Mji wa Sihoni na ujengwe na kuthibitishwa;

28 Yer 48:45-46; Isa 15:4; Kum 2:9; Isa 15:1 Maana, moto umetoka Heshboni,

Umekuwa Ari ya Moabu,

Mwali wa moto umetoka mji wa Sihoni;

Wakuu wa mahali palipoinuka Arnoni.

29 Amu 11:24; 1 Fal 11:7,33 Ole wako Moabu!

Umeangamia, enyi watu wa Kemoshi;

Amewatoa wanawe kuwa wakimbizi,

Na binti zake waende utumwani,

Wamwendee Sihoni mfalme wa Waamori.

30 Yer 48:18,22 Tumewapigia mishale; Heshboni umepotea mpaka Diboni,

Nasi tumeharibu mpaka Nofa,

Ifikiayo Medeba.

31Basi hivyo Israeli akaketi katika nchi ya Waamori.

32Yer 48:32 Kisha Musa akatuma watu ili kupeleleza Yazeri, nao wakaitwaa miji yake, wakawafukuza Waamori waliokuwamo.

Kushindwa kwa mfalme wa Ogu vitani

33 Yos 13:12 Kisha wakageuka na kukwea kwa njia ya Bashani; na Ogu mfalme wa Bashani akaondoka apigane nao huko Edrei, yeye na watu wake wote.

34Kum 3:2; Zab 135:10; 136:20 BWANA akamwambia Musa, Usimwogope; kwa kuwa nimekwisha mtia mkononi mwako, na watu wake wote, na nchi yake; nawe utamtenda kama ulivyomtenda Sihoni mfalme wa Waamori, aliyeishi Heshboni.

35Kum 3:3,4 Basi wakampiga, na wanawe, na watu wake wote, hata wasibakize kwake mtu yeyote; nao wakaimiliki nchi yake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help