Zaburi 113 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Mungu msaidizi wa mhitaji

1Haleluya.

Enyi watumishi wa BWANA, sifuni,

Lisifuni jina la BWANA.

2 Dan 2:20 Jina la BWANA lihimidiwe

Tangu leo na hata milele.

3 Isa 59:19; Hab 2:14; Mal 1:11; Ufu 11:15 Toka mawio ya jua hata machweo yake

Jina la BWANA husifiwa.

4BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote,

Na utukufu wake ni juu ya mbingu.

5Ni nani aliye mfano wa BWANA,

Mungu wetu aketiye juu;

6 Isa 57:15 Anyenyekeaye kutazama,

Mbinguni na duniani?

7 1 Sam 2:8; Isa 26:19; Dan 12:2 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,

Na kumpandisha maskini kutoka jaani.

8 Ayu 36:7 Ili amketishe pamoja na wakuu,

Pamoja na wakuu wa watu wake.

9 1 Sam 2:5; Gal 4:27 Humweka nyumbani mwanamke aliye tasa,

Awe mama wa watoto, mwenye furaha.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help