1 Mwa 21:31; 26:24; 28:13; 31:42 Israeli Akasafiri, pamoja na yote aliyokuwa nayo, akaja Beer-sheba, akamchinjia sadaka Mungu wa Isaka babaye.
2Mwa 15:1; Ayu 33:14,15 Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. Akasema, Mimi hapa.
3Mwa 12:2; 28:13; Kum 26:5; Kut 1:9 Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko.
4Mwa 28:15; 48:21; 15:16; 50:13; Kut 3:8 Mimi nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha tena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako.
5Mwa 15:13; Mdo 7:15 Yakobo akaondoka Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao na watoto wao wadogo, na wake zao katika magari aliyotuma Farao ili kumchukua.
6Kum 26:5; Yos 24:4; Zab 105:23; Isa 52:4 Wakatwaa na wanyama wao, na mali zao walizokuwa wamepata katika nchi ya Kanaani, wakaja Misri, Yakobo na uzao wake wote pamoja naye.
7Wanawe, na wana wa wanawe, pamoja naye, binti zake na binti za wanawe, na uzao wake wote, aliwaleta pamoja naye mpaka Misri.
8 Kut 1:1; 6:14; Hes 26:5; 1 Nya 5:1 Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli walioingia Misri, Yakobo na wanawe: Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo.
9Na wana wa Reubeni; Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi.
10Kut 6:15; 1 Nya 4:24 Na wana wa Simeoni; Yemueli na Yamini, na Ohadi, na Yakini, na Sohari, na Shauli, mwana wa mwanamke Mkanaani.
11Na wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.
12Mwa 38:3,29; 1 Nya 2:5 Na wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela, na Peresi, na Zera; lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani. Na wana wa Peresi, ni Hesroni, na Hamuli.
13Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni.
14Na wana wa Zabuloni; Seredi, na Eloni, na Yaleeli.
15Hao ndio wana wa Lea, aliomzalia Yakobo katika Padan-aramu, na Dina, binti yake. Wanawe wote wa kiume na kike walikuwa watu thelathini na watatu.
16Hes 26:15 Na wana wa Gadi; Sefoni, na Hagi, na Shuni, na Esboni, na Eri, na Arodi, na Areli.
171 Nya 7:30 Na wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na Sera, dada yao. Na wana wa Beria ni Heberi, na Malkieli.
18Mwa 30:10 Hao ndio wana wa Zilpa, ambaye Labani alimpa Lea, binti yake, naye akamzalia Yakobo hao, watu kumi na sita.
19Wana wa Raheli, mkewe Yakobo, Yusufu na Benyamini.
20Mwa 41:50-52 Walizaliwa kwake Yusufu katika nchi ya Misri, Manase na Efraimu, aliomzalia Asenathi binti Potifera, kuhani wa Oni.
211 Nya 7:6,12 Na wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Ashbeli, na Gera, na Naamani, na Ehi, na Roshi, na Mupimu, na Hupimu, na Ardi.
22Hao ndio wana wa Raheli, aliomzalia Yakobo, wote walikuwa watu kumi na wanne.
231 Nya 7:12 Na wana wa Dani; Hushimu.
241 Nya 7:13 Na wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yaseri, na Shilemu.
25Mwa 29:29; 30:5,7 Hao ndio wana wa Bilha, ambaye Labani alimpa Raheli, binti yake, naye akamzalia Yakobo hao; wote walikuwa watu saba.
26 Kut 1:5 Watu wote waliokuja pamoja na Yakobo mpaka Misri, waliokuwa wazao wake, bila wake za wanawe, walikuwa watu sitini na sita.
27Mdo 7:14; Kum 10:22 Na wana wa Yusufu aliozaliwa katika Misri walikuwa wawili. Watu wote wa nyumba ya Yakobo walioingia Misri walikuwa sabini.
Yakobo apata makao Gosheni28 Mwa 31:21 Yakobo akamtuma Yuda mbele yake kwa Yusufu, ili amwongoze njia mpaka Gosheni. Wakaja mpaka nchi ya Gosheni.
29Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli, babaye, huko Gosheni; akajionesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake kitambo kirefu.
30Lk 2:29 Israeli akamwambia Yusufu, Na nife sasa, kwa kuwa nimekuona uso wako, ya kuwa ungali hai.
31Yusufu akawaambia ndugu zake na watu wa nyumbani mwa baba yake, Nitapanda mimi nimpashe Farao habari; nitamwambia, Ndugu zangu, na watu wa nyumbani mwa baba yangu, waliokuwa katika nchi ya Kanaani, wamenijia.
32Na watu hao ni wachungaji, maana wamekuwa watu wa kuchunga wanyama, nao wameleta kondoo zao, na ng'ombe zao, na yote waliyo nayo.
33Mwa 47:2,3 Itakuwa Farao atakapowaita, na kuwauliza, Kazi yenu ni nini?
34Mwa 30:35; 34:5; 37:12; Kut 8:26 Semeni, Watumishi wako tumekuwa wachunga wanyama tangu ujana wetu, na hata leo, sisi, na baba zetu; mpate kukaa katika nchi ya Gosheni; maana kila mchunga wanyama ni chukizo kwa Wamisri.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.