Yohana 13 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Yesu awaosha wanafunzi miguu

1 hana haja ila ya kuosha miguu, maana yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote.

11Yn 6:64,70,71 Kwa maana alimjua yeye atakayemsaliti; ndiyo maana alisema, Si nyote mlio safi.

12 Lk 22:27 Basi alipokwisha kuwaosha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa hayo niliyowatendea?

13Mt 23:8,10 Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.

14Lk 22:27; 1 Tim 5:10 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewaosha miguu, imewapasa ninyi pia kuoshana miguu ninyi kwa ninyi.

15Flp 2:5; Kol 3:13; 1 Pet 2:21 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.

16Mt 10:24; Lk 6:40; Yn 15:20 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyemtuma.

17Mt 7:24; Yak 1:25 Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.

18Zab 41:9 Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa,

Aliyekula chakula changu

Ameniinulia kisigino chake.

19 Yn 14:29 Tangu sasa nawaambia kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye.

20Mt 10:40; Mk 9:37; Lk 9:48; 10:16 Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeaye mtu yeyote nimtumaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi; ampokea yeye aliyenituma.

Yesu atabiri juu ya kusalitiwa kwake

21 Mt 26:21-25; Mk 14:18-21; Lk 22:21-23 Naye alipokwisha kusema hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia akisema, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti. Yn 12:27

22Wanafunzi wakatazamana, huku wakiwa na mashaka ni nani amnenaye.

23Yn 19:26; 20:2; 21:7,20 Na palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda.

24Basi Simoni Petro akampungia mkono, akamwambia, Uliza, ni nani amtajaye?

25Basi yeye, huku akimwelekea Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani?

26Basi Yesu akajibu, Ndiye mtu yule nitakayemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akalitwaa akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti.

27Yn 13:2 Na baada ya hilo tonge Shetani alimwingia. Basi Yesu akamwambia, Uyatendayo yatende upesi.

28Wala hakuna mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua sababu ya kumwambia hivyo.

29Yn 12:6 Kwa maana wengine walidhania, kwa kuwa Yuda huchukua mfuko, ya kwamba Yesu alimwambia kama, Nunua mnavyovihitaji kwa sikukuu; au kwamba awape maskini kitu.

30Basi huyo, akiisha kulipokea lile tonge, akatoka mara hiyo. Nako kulikuwa ni usiku.

Amri mpya

31Basi huyo alipokwisha kutoka, Yesu alisema, Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, naye Mungu ametukuzwa ndani yake.

32Yn 12:23; 17:1-5 Mungu naye atamtukuza ndani ya nafsi yake; naye atamtukuza mara.

33Yn 7:34; 8:21 Enyi watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta; na kama vile nilivyowaambia Wayahudi ya kwamba, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja; kadhalika sasa nawaambia ninyi.

34Yn 15:12,13,17; 3:23; 2 Yoh 1:5; 1 Yoh 2:8,10 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.

35Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.

Yesu atabiri kuwa Petro atamkana

36 Mt 26:33-35; Mk 14:29-31; Lk 22:31-34 Simoni Petro akamwambia, Bwana, unakwenda wapi? Yesu akamjibu, Niendako huwezi kunifuata sasa; lakini utanifuata baadaye. Yn 7:34; 21:18,19

37Petro akamwambia, Bwana, kwa nini mimi nisiweze kukufuata sasa? Mimi nitautoa uhai wangu kwa ajili yako.

38Yesu akamjibu, Je! Wewe utautoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin, nakuambia, Jogoo hatawika hadi wewe utakapokuwa umenikana mara tatu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help