Zaburi 13 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Sala ya ukombozi kutoka kwa aduiKwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 Kum 31:17; Ayu 13:24; Zab 22:1; Isa 59:2 Ee BWANA, utanisahau hadi lini, hata milele?

Hadi lini utanificha uso wako?

2Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini,

Nikihuzunika moyoni mchana kutwa?

Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini?

3 Ezr 9:8; Zab 18:28; Lk 2:32; Ufu 21:23; Zab 76:5,6; Isa 37:36; Yer 51:39; Efe 5:14 Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie;

Uyatie nuru macho yangu,

Nisije nikalala usingizi wa mauti.

4Adui yangu asije akasema, Nimemshinda;

Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.

5 2 Nya 20:12 Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako;

Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.

6Naam, nitamwimbia BWANA,

Kwa kuwa amenitendea kwa ukarimu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help