Hesabu 5 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Watu najisi

1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

2 kambini, na kila mtu aliye na kisonono, na kila aliye najisi kwa ajili ya maiti;

3 asitie mafuta juu yake, wala asitie ubani juu yake; maana, ni sadaka ya unga ya wivu, ni sadaka ya unga ya ukumbusho ya kukumbukia uovu.

16Law 1:3; Yer 17:10; 1 Nya 28:9; Mal 3:5; Ebr 13:4 Basi kuhani atamleta mwanamke akaribie, na kumweka mbele za BWANA;

17kisha kuhani atatwaa maji matakatifu katika chombo cha udongo; kisha kuhani atatwaa katika vumbi lililo pale chini ya maskani, na kulitia katika hayo maji;

18kisha kuhani atamweka mwanamke mbele za BWANA, naye atazifungua nywele za kichwani mwa huyo mwanamke, kisha atampa hiyo sadaka ya unga ya ukumbusho mikononi mwake, ambayo ni sadaka ya unga ya wivu, naye kuhani atakuwa na hayo maji ya uchungu yaletayo laana mkononi mwake;

19tena kuhani atamwapisha huyo mwanamke, naye atamwambia mwanamke, Kwamba hakulala mtu mume pamoja nawe, tena ikiwa hukukengeuka kutenda maovu, ukiwa chini ya mumeo, maji haya ya uchungu yaletayo laana yasikudhuru;

20lakini ikiwa umekengeuka ukiwa chini ya mumeo, na kwamba u hali ya unajisi, na mwanamume amelala nawe, asiyekuwa mumeo;

21Mwa 9:25; Yos 6:26; 1 Sam 14:24; Neh 10:29; Mal 4:6; Mt 26:74; Isa 65:15; Yer 29:22 hapo ndipo kuhani atamwapisha mwanamke kwa kiapo cha kuapiza, kisha kuhani atamwambia huyo mwanamke maneno haya, BWANA na akufanye wewe uwe laana na kiapo kati ya watu wako, hapo BWANA akufanyapo paja lako kupooza, na tumbo lako kuvimba;

22Zab 109:18; Mit 1:31; Eze 3:3; Kum 27:15 na maji yaletayo laana yatakuingia matumboni mwako, na kukuvimbisha tumbo, na kukupoozesha paja lako; na mwanamke ataitika, Amina, Amina.

23Kisha kuhani ataziandika laana hizo ndani ya kitabu, na kuzifuta katika maji ya uchungu;

24kisha atamnywesha mwanamke hayo maji ya uchungu yaletayo laana; nayo maji yaletayo laana yataingia ndani yake, nayo yatageuka kuwa uchungu.

25Kut 29:24; Law 8:27 Kisha kuhani ataitwaa hiyo sadaka ya unga ya wivu, kwa kuiondoa mkononi mwa huyo mwanamke, naye ataitikisa sadaka ya unga mbele za BWANA, na kuisongeza pale madhabahuni;

26Law 2:2,9 kisha kuhani atatwaa konzi moja ya sadaka ya unga, kuwa ni ukumbusho wake, na kuuteketeza madhabahuni, baadaye atamnywesha mwanamke hayo maji.

27Kum 28:37; Zab 83:9; Mhu 7:26; Isa 65:15; Yer 24:9; Zek 8:13 Kisha hapo atakapokwisha kumnywesha maji, ndipo itakapokuwa, kama amekuwa hali ya unajisi na kumkosea mumewe, hayo maji yaletayo laana yatamwingia ndani yake, nayo yatakuwa uchungu, na tumbo lake litavimba, na paja lake litapooza; na huyo mwanamke atakuwa laana kati ya watu wake.

28Ayu 17:8,9; Zab 37:5,6; Rum 5:3-5 Na kama mwanamke hakuwa na unajisi lakini yu safi; ndipo ataachiliwa, naye atazaa wana.

29Hii ndiyo sheria ya wivu, mwanamke, ambaye yu chini ya mumewe, akikengeuka, na kupata unajisi;

30au, roho ya wivu ikimwingia mtu mume, naye akamwonea wivu mkewe; ndipo atakapomweka huyo mwanamke mbele za BWANA, na kuhani atatenda juu yake sheria hii yote.

31Law 20:17; Eze 18:4; Rum 2:8,9 Na huyo mume atakuwa hana uovu, na mwanamke atauchukua uovu wake.

Blog
About Us
Message
Site Map