Mika 1 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

1 2 Pet 1:21; Yer 26:18; 2 Fal 15:32–16:20; 18:1–20:21; 2 Nya 27:1-7; 28:1–32:33 Hili ndilo neno la BWANA lililomjia Mika, Mmoreshathi, katika siku za Yothamu, na Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda; maono aliyoyaona kuhusu Samaria na Yerusalemu.

Hukumu yatangazwa juu ya Samaria

2Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu.

3Isa 26:21; Eze 3:12; Ebr 12:18,19 Kwa maana, angalieni, BWANA anakuja akitoka mahali pake, naye atashuka, na kupakanyaga mahali pa dunia palipoinuka.

4Na hiyo milima itayeyuka chini yake, nayo mabonde yatapasuliwa, kama vile nta iliyo mbele ya moto, kama maji yaliyomwagika katika mteremko.

5Yer 2:18,19; Hos 5:5 Kwa sababu ya kosa la Yakobo yametokea haya yote, na kwa sababu ya makosa ya nyumba ya Israeli. Nini kosa la Yakobo? Je, silo Samaria? Na nini mahali pa Yuda palipoinuka? Sipo Yerusalemu?

62 Fal 19:25 Kwa ajili ya hayo nitafanya Samaria kuwa kama chungu katika shamba, na kama miche ya shamba la mizabibu; nami nitayatupa mawe yake bondeni, nami nitaifunua misingi yake.

7Na sanamu zake zote za kuchonga zitapondwapondwa, na ijara zake zote zitateketezwa kwa moto, na sanamu zake zote nitazifanya ukiwa; kwa kuwa amezikusanya kwa ujira wa kahaba, nazo zitaurudia ujira wa kahaba.

Maangamizi ya miji ya Yuda

8Kwa ajili ya hayo nitaomboleza na kulia,

Nitakwenda nimevua nguo, nikiwa uchi;

Nitaomboleza kama mbweha,

Na kulia kama mbuni.

9 2 Fal 18:13 Kwa maana majeraha yake hayaponyeki;

Maana msiba umeijia hata Yuda,

Unalifikia lango la watu wangu,

Naam, hata Yerusalemu.

10Msiyahubiri haya katika Gathi, msilie kamwe;

Katika Beth-le-Afra ugaegae mavumbini.

11Piteni; njia yenu, wakazi wa Shafiri, mkiwa uchi na wenye aibu;

Wakazi wa Saanani msijitokeze nje;

Beth-eseli unalia

na ataondoa msaada wake kwenu;

12Maana wakazi wa Marothi wanasubiri kwa hamu kupata mema;

Lakini maangamizi yameshuka toka kwa BWANA,

Yamefika katika lango la Yerusalemu.

13Mfungie gari la vita farasi

Aliye mwepesi, wakazi wa Lakishi;

Alikuwa mwanzo wa dhambi kwa binti Sayuni;

Maana makosa ya Israeli yameonekana kwako.

14Kwa hiyo mtaipa Moresheth-Gathi zawadi ya kuagia;

Nyumba za Akzibu zitakuwa kijito kidanganyacho wafalme wa Israeli.

15Bado, wakazi wa Maresha, nitawaleteeni tena yeye atakayewamiliki;

Utukufu wa Israeli utafika Adulamu.

16 2 Fal 17:6 Jinyoeni upara, jikateni nywele zenu,

Kwa ajili ya watoto waliowafurahisha;

Panueni upara wenu kama tai;

Kwa maana wamekwenda mbali nanyi uhamishoni.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help