Zaburi 24 - Bible in Kiswahili, Revised Union Version 2013

Kuingia hekaluniYa Daudi. Zaburi.

1 1 Kor 10:26; Kut 9:29; Ayu 41:11 Nchi na vyote vilivyomo ni mali ya BWANA,

Dunia na wote wakaao ndani yake.

2Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari,

Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.

3Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA?

Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?

4 Mt 5:8 Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe,

Asiyeiweka nafsi yake katika uongo,

Wala hakuapa kwa hila.

5Atapokea baraka kwa BWANA,

Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.

6Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao,

Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.

7 Hag 2:7; Mal 3:1; 1 Kor 2:8 Inueni vichwa vyenu, enyi malango,

Inukeni, enyi malango ya milele,

Mfalme wa utukufu apate kuingia.

8Ni nani Mfalme wa utukufu?

BWANA mwenye nguvu, hodari,

BWANA hodari wa vita.

9Inueni vichwa vyenu, enyi malango,

Naam, viinueni, enyi malango ya milele,

Mfalme wa utukufu apate kuingia.

10Ni nani huyu Mfalme wa utukufu?

BWANA wa majeshi,

Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help